Home news WAKATI DILI LAKE NA MAZEMBE LIKIFA NJIANI…YANGA WAFUNGUKA HATMA YA MUKOKO…WAGUSIA MKATABA...

WAKATI DILI LAKE NA MAZEMBE LIKIFA NJIANI…YANGA WAFUNGUKA HATMA YA MUKOKO…WAGUSIA MKATABA WAKE..


Klabu ya Young Africans imethibitisha kurejea kwa kiungo kutoka DR Congo Mukoko Tomombe akitokea nchini kwao.

Tomombe amerejea Tanzania, baada ya dili lake la kujiunga na TP Mazembe kwa mkopo kukwama mwishoni mwa juma lililopita.

Young Africans walidhamiria kumtoa kwa mkopo kiungo huyo, kama sehemu ya kumpata Kiungo Mshambuliaji Chico Ushindi, ambaye tayari ameshatua Jangwani akitokea TP Mazembe.

Tomombe amejiunga na wenzake Jijini Arusha ambapo kikosi cha Young Africans kimeweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Mzunguuko wa 13 dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa mwishoni mwa juma hili Mjini Moshi-Kilimanjaro, Uwanja wa Ushirika.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo Hassan Bumbuli amesema Tomombe amerejea na bado ni mchezaji halali wa Young Africans.

β€œMukoko amejiunga nasi hapa Arusha tangu jana, atakuwa sehemu ya kikosi chetu kwa mujibu wa mkataba wake.”

β€œTaarifa nyingine kuhusu Mukoko zitatolewa baadae lakini ifahamike kuwa bado ni mchezaji wetu,” amesema Bumbuli.

SOMA NA HII  HATIMA YA MAYELE NA YANGA IKO HIVI...ATAKA MSHAHARA WA MILI 53 KWA MWEZI...ADA YA USAJILI BIL 1...