Home Azam FC BAADA YA KUHAKIKISHIWA MAISHA …KOCHA MMAREKANI WA AZAM FC AITAJA SIMBA..AANIKA HAYA..

BAADA YA KUHAKIKISHIWA MAISHA …KOCHA MMAREKANI WA AZAM FC AITAJA SIMBA..AANIKA HAYA..


KOCHA Mkuu wa Azam raia wa Marekani,  Abdi Hamid Moallin ameweka wazi kuwa kipaumbele chake kikubwa mara baada ya kurasimishwa kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho, ni kuhakikisha wanashinda ubingwa wa Kombe la Shirikisho laAzam (FA) linalotetewa na Simba.

Moallin alitangazwa rasmi kuchukua majukumu ya ukocha mkuu ndani ya kikosi chaAzam

Januari 25, mwaka huu mara baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa mafanikio kama kaimu kocha mkuu tangu Desemba mwaka jana.

Tayari chini yakeAzam kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho laAzam wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora dhidi ya Transit Camp, ambapo sasa watavaana na Baga Friends.

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Moallin alisema: “Ni jambo zuri kuona kikosi chetu kimefanikiwa kufika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho, tunayo malengo mengi kama timu msimu huu.

“Lakini lengo kubwa la muda mfupi ni kuhakikisha tunapata nafasi ya kucheza fainali ya michuano hii na kutwaa ubingwa, ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kucheza mashindano ya kimataifa mwakani.”

SOMA NA HII  CHAMA AITEKA SOKOINE...UWANJA MZIMA WALIPUKA JINA LAKE..PABLO AWAKATA MAINI...