Home news BAADA YA KUONA HAOMBI MSAMAHA WALA HANA SHIDA…SIMBA WAMCHIMBWA MKWARA WA KUFA...

BAADA YA KUONA HAOMBI MSAMAHA WALA HANA SHIDA…SIMBA WAMCHIMBWA MKWARA WA KUFA MTU MORRISON…


UNAAMBIWA KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morisson, mpaka Feb 8, 2022 hakuwa ameandika barua ya maelezo baada ya kutakiwa kuandika kujibu makosa ya kinidhamu yanayomkabili huku uongozi ukimchimba mkwara kama akiendelea kuchelewa atapelekwa kamati ya nidhamu.

Kiungo huyo ambaye alitimka nchini kwenda kwao Ghana ikiwa ni muda mfupi baada ya kusimamishwa alitua nchini usiku wa kuamkia juzi Jumanne na uongozi wa Simba umemkumbusha kuwa anatakiwa kuandika barua hiyo la sivyo hatocheza mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Asec Mimosas Jumapili hii.

Morrison ambaye mpaka sasa hayupo kambini baada ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kile kilicholezwa kuwa mtovu wa nidhamu, kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa kurudi kuichezea Yanga.

Hivi karibuni, wakati Simba ikitangaza kumsimamisha nyota huyo raia wa Ghana, taarifa yao ilibainisha kwamba lazima aandike barua ya maelezo kwenda kwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez.

Lakini inaelezwa kuwa, kiungo huyo yupo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga wenye thamani ya Sh 230Mil.

Akizungumza na  gazeti la Championi Jumatano, Meneja Habari wa timu hiyo, Ahmed Ally Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema: “Kwanza kabisa ijulikane kuwa Morrison ni mchezaji halali wa Simba mwenye mkataba, yeye amerejea nchini leo (jana) usiku akitokea kwao Ghana.

“Mpaka leo (jana) asubuhi, Morrison bado hajatuma barua ya aina yoyote ile ya kujieleza makosa yake kwa uongozi labda hapo baadaye huenda akatuma barua hiyo.

“Kama hataweza kutuma haraka barua hiyo na kamati kuamua hukumu yake, basi ataukosa mchezo wetu ujao dhidi ya Asec Mimosas,” alisema Ahmed na kuongeza kuwa: “Suala lake limefikia katika hatua hiyo kwa hivi sasa, lakini kama akiendelea kugoma kuandika barua basi litapelekwa katika kamati ya nidhamu ya timu Simba kwa ajili ya kumjadili kabla ya maamuzi mengine kuchukuliwa.”

SOMA NA HII  FT: SIMBA SC 5 - 0 MTIBWA SUGAR ....SAKHO AIBUKA NA STAILI MPYA...AKPAN AKUMBUKWA...