Home Habari za michezo KUMBE ALIYEWATIA UCHUNGU SIMBA JUZI NI ‘MCHEZAJI WA NDONDO’…HANA MKATABA NA MLANDEGE..

KUMBE ALIYEWATIA UCHUNGU SIMBA JUZI NI ‘MCHEZAJI WA NDONDO’…HANA MKATABA NA MLANDEGE..

Habari za Simba leo

Simba haitamsahau kiungo mshambuliaji Joseph Akandwanaho ambaye amewanyima taji la tano la ubingwa wa Mapinduzi lakini kumbe jamaa wala hakuwa na mkataba na sasa ana dili zito mezani.

Akandwanaho hakuwa sehemu ya kikosi cha Mlandege wakati timu hiyo inacheza mechi zake tano zilizopita kabla ya fainali kuanzia hatua ya makundi.

Ghafla akaibuka kwenye mchezo wa fainali na kuwaumiza Simba kwa bao hilo pekee ambalo aliwafanyia kitu mbaya mabeki wa Wekundu hao.

Kiungo huyo alikuwa bado hajasajiliwa na Mlandege mpaka anaingia kwenye mchezo huo akichukuliwa kutoka Mbarara City inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda.

Meneja wa mchezaji huyo ambaye hakutaka kutajwa kwa jina lake ameliambia Mwanaspoti kuwa Akandwanaho alikuwa anajaribiwa na Mlandege ili wampe mkataba ambapo sasa simu zimeshakuwa nyingi klabu mbalimbali zikiwania saini yake.

“Bado hajapewa mkataba na Mlandege huu ndio mchezo wake wa kwanza tulipofika mazoezini kocha akampenda na akaomba wamtumie kwenye mchezo huu wa fainali,”alisema meneja wa mchezaji huyo ambaye ni raia wa Uganda pia.

“Tangu jana mchezo ulipokwisha simu zimekuwa nyingi sana hata klabu yake ya Mbarara nayo imeshtuka kumuona huku ingawa kwenye mkataba wake na klabu hiyo unamruhusu kuondoka kwenda kwenye majaribio.”

SOMA NA HII  AZIZ KI ALIVYOITESA YANGA KWA DAKIKA 356....ISHU NZIMA IKO HIVI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here