Home Azam FC BAADA YA KUSHINDWA KUFURUKUTA CAMEROON NA TIMU YA TAIFA…PRINCE DUBE AIBUKA NA...

BAADA YA KUSHINDWA KUFURUKUTA CAMEROON NA TIMU YA TAIFA…PRINCE DUBE AIBUKA NA HILI KWA AZAM…


BAADA ya kupitia kipindi kigumu cha kuandamwa na majeraha, hatimaye straika wa Azam FC, Prince Dube, amesema kuwa kwa sasa yupo fiti, anataka kupambana na kuifungia mabao mengi timu yake.

Dube amesema msimu uliopita alipishana na kiatu cha ufungaji bora kwa sababu alikuwa anaumia mara kwa mara, lakini kwa sasa yupo fiti na anarudi akiwa na nguvu kubwa uwanjani.

Akizungumzia hali yake kiafya na mwenendo wa ligi tangu kuanza kwa msimu huu, Dube alisema kumekuwa na mabadiliko makubwa kwa timu nyingi na ushindani umeongezeka, ila kwa kuwa amepona na kuwa fiti, atafanya kile mashabiki wake wanataka.

“Msimu niliuanza vibaya kutokana na majeraha. Niliumia sana kwa sababu malengo yalikuwa ni kuisaidia timu ila nashukuru nimerejea na nipo tayari kwa hilo,” alisema.

SOMA NA HII  ISHU YA KUWA KOCHA MKUU KABISA...AHMED ALLY 'AMSILIBIA DOLE GUMBA MGUNDA' ...ADAI TIMU ILIKUWA HAIPAMBANI...