Home news EXCLUSIVE….KUMBE SIMBA WALIKUBALI KUMSAMEHE MORRISON KWA MASHARTI HAYA MAWILI…

EXCLUSIVE….KUMBE SIMBA WALIKUBALI KUMSAMEHE MORRISON KWA MASHARTI HAYA MAWILI…

 


UONGOZI wa Simba licha ya kumsamehe winga wao, Bernard Morrison, lakini wamepatia masharti ambayo anatakiwa kuyafuata baada ya kupewa msamaha huo ndani ya kikosi chao.

Morrison alisimamishwa ndani ya timu hiyo kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu alivyoonyesha huku uongozi wa Simba ukimtaka mchezaji huyo kuandika barua ya maelezo kwenda kwa CEO wa timu hiyo, Barbara Gonzalez jambo ambalo Morrison alilitekeleza

 Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally alisema kuwa tayari uongozi wa timu hiyo umepokea barua ya maelezo ambapo mchezaji huyo aliomba msamaha kwa maandishi na maneno baada ya kukutana na uongozi wa Simba ambao baada ya kumsamehe umempa masharti ya kuwa mfano mzuri wa kuigwa ndani ya timu hiyo na kutorudia vitendo vya utovu wa nidhamu.

“Jumatatu mchana Bernard Morrison aliwasilisha barua ya msamaha kwa uongozi wa Simba ambapo alikutana na uongozi wa timu wakazungumza na Morrison alipatiwa msamaha na siku hiyohiyo alijiunga na wenzake na kuanza rasmi mazoezi.

“Katika msamaha ambao amepewa winga huyo anatakiwa kuacha kufanya tena vitendo vya utovu wa nidhamu na kuwa mfano wa kuigwa kwa wachezaji wengine ambapo mwenyewe amekiri kuwa atafanya hivyo na kuwa mfano bora wa kuigwa na kucheza kwa kujituma ndani ya timu hiyo,” alisema kiongozi huyo.

SOMA NA HII  ATUMIA MIL 56 KUNUNUA MBWA WA KULINDA MEDALI ZAKE ZA KOMBE LA DUNIA...