Home news HUU HAPA UKWELI KUHUSU SABABU YA MAKATA KUTIMULIWA DODOMA JIJI…

HUU HAPA UKWELI KUHUSU SABABU YA MAKATA KUTIMULIWA DODOMA JIJI…


TAARIFA rasmi kutoka kwenye klabu ya Dodoma Jiji, imethibitisha kumfungashia virago, aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbwana Makata kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.

Ndani ya michezo mitano iliyopita, Makata alijikuta akiongoza Dodoma Jiji kuambulia pointi moja tu dhidi ya Geita Gold na kukumbana na vipigo vinne, ikiwemo vitatu mfululizo ambavyo ni kama vilikoleza kuota nyasi kwa kibarua chake makao makuu ya nchi.

Taarifa rasmi iliyotolewa leo, Jumatano imeeleza kuwa,”Hatua hizi zimechukuliwa kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo ya timu katika mashindano mbalimbali ya msimu huu wa 2021/22.”

SOMA NA HII  LICHA YA KUIBUKA NA GOLI 5 ...HIZI HAPA REKODI ZA KIBABE ZILIZOWEKWA NA SIMBA JANA..