Home Ligi Kuu SEKUNDE CHACHE KABLA YA MECHI…NABI AWABADILISHIA MTIBWA GIA ANGANI..ALIA NA UWANJA WA...

SEKUNDE CHACHE KABLA YA MECHI…NABI AWABADILISHIA MTIBWA GIA ANGANI..ALIA NA UWANJA WA MANUNGU..


MECHI ya kisasi! Ndivyo utakavyosema katika kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaozikutanisha Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga utakaopigwa leo saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Timu hizo zitavaana katika mchezo wa kwanza wa ligi, lakini Mtibwa wataingia uwanjani wakitaka kulipa kisasi cha kufungwa katikamchezo wa mwisho msimu uliopita bao 1-0 lililofungwa na kiungo mshambuliaji raia wa Angola, Fernandos Carinhos.

Wakati Mtibwa wakiingia kutaka kulipa kisasi, Yanga wenyewe wanahitaji pointi  tatu ili waendelee kukaa kileleni kwa kuwaacha watani wake kwa gepu kubwa la pointi katika msimamo wa ligi.

Yanga inaongoza katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 36 ikifuatiwa na watani wao Simba wenye 31 huku Mtibwa 12 wakiwa katika nafasi ya 14.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nasreddine Nabi alisema kuwa anafahamu anakwenda kucheza mchezo mgumu dhidi ya Mtibwa huku akiwa amekiandaa kikosi chake kukabiliana na changamoto zote watakazokutana nazo.

Nabi alisema kuwa moja ya changamoto anayokwenda kukutana nayo ni ubovu wa uwanja, ambao kwake hataki iwe sababu ya kupoteza mchezo huo muhimu kwao kupata matokeo mazuri.

Alisema kuwa siku tatu alizotumia kukiandaa kikosi chake kambini Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam, zimetosha vijana wake kupata matokeo mazuri, licha ya changamoto ya uwanja watakayokutana nayo.

“Nimeki– andaa kikosi changu kutokana na aina ya uwanja  nitakaokwenda kuutumia dhidi ya Mtibwa, siufahamu lakini nimepata taarifa za uwanja huo.

“Mimi ninakiandaa kikosi changu katika mazingira yote, kwani uzuri nafahamu changamoto iliyopo hapa nchini ya viwanja,uzuri vijana wangu wanafahamu vizuri hivyo sina hofu, tumejiandaa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri, licha ya kukabiliwa na majeraha kikosini kwangu,”alisema Nabi.

Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Mtibwa, Awadh Juma, alisema: “Maandalizi yapo vizuri na wachezaji wana morali kubwa ya kupata matokeo mazuri.

“Tunashukuru namba ya wachezaji waliokuwa wana majeraha imepungua, tunaamini kwetu yatakuwa mazingira rafiki kutokana na kutumia uwanja wa nyumbani.

SOMA NA HII  CHEZA BUREE NA USHINDE KUPITIA CASINO ZA MERIDIANBET....

“Morali ipo juu kwa wachezaji wetu wote, hivi sasa tunawatengeneza kisaikolojia tu kutokana na ukubwa wa mchezo huu, kwani mazoezi ni yaleyale wanay– ofanya kila siku,” alisema Juma.