Home news IMEFICHUKAA…BAADA YA YANGA KUMKOSA MOSES PHIRI..KUMBE WALIAMUA KULIAMSHA KWA BM..MESEJI ZANASWA….

IMEFICHUKAA…BAADA YA YANGA KUMKOSA MOSES PHIRI..KUMBE WALIAMUA KULIAMSHA KWA BM..MESEJI ZANASWA….


IMEFICHUKA buana. Klabu ya Simba juzi jioni ilitangaza kumsimamisha kwa muda usiojulikana winga wake kutoka Ghana, Bernard Morrison, lakini gazeti la Mwanaspoti limepenyezewa kila kitu juu ya kilichomponza nyota huyo.

Katika taarifa ya uongozi wa klabu hiyo, nyota huyo ametakiwa kutoa maelezo ya kimaandishi kwa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na iwapo atashindwa hatua zaidi za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

Licha ya taarifa za uongozi wa Simba kueleza utoro kambini wa kila mara kwa winga huyo, lakini chanzo cha ndani kutoka klabu hiyo zinasema kuwa mbali na utukutu huo, lakini inaelezwa mawasiliano ya siri baina yake na mabosi wa klabu yake ya zamani wa Yanga ni moja ya sababu ya kilichosababishwa apigwe ‘stop’.

Chanzo hicho kilichokataa kuandikwa jina  kilisema, wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi 2022 iliyofanyika Zanzibar, mabosi wa Simba walibaini kuwepo kwa mawasiliano ya sri baina ya Mghana huyo na vigogo wa Yanga.

Inaelezwa, mabosi wa Yanga walikuwa wakichati na Morrison wakimjaza upepo kwamba wanataka kumrudisha kikosini, licha ya kuwabwaga kwenye kesi iliyokaa kwa muda mrefu katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS).

Morrison aliburuzwa na Yanga baada ya kuukana mkataba unaodaiwa alisaini Jangwani, baada ya Simba kumshawishi kujiunga nao wakati akimalizia mkataba wake wa miezi sita na TFF kupitia kamati zake kumuidhinisha Msimbazi.

“Mwanzoni tulijua ni ishu zake za kifamilia zilizokuwa zikimchanganya kiasi cha kusumbua kujiunga na kambi, lakini tulibaini jamaa alikuwa akiwasiliana na watu wa upande wa pili, huku akitoroka kila mara kambini japo alikuwa akionywa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Hofu yetu ni kwamba huenda kuna siri zinaweza kuwa zinavujia kwa wenzetu, hivyo kufanya uongozi uchukue hatua za haraka kumsimamisha. Nikwambie tu huyu jamaa tumemuangalia muda mrefu sana, kutokana na tabia zake, lakini tukawa tunamsema ili abadilike lakini  imeshindikana.”

“Ni mara nyingi viongozi tunaambiwa matukio yake kutoka huko kambini, mpaka tunajiuliza huyu jamaa ana shida gani,” kilisisitiza chanzo hicho, kilichoeleza pia kuna wakati winga huyo alikuwa akigoma kula chakula na wenzake.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO MASTAA YANGA WALIVYOJIGAWIA TIMU ZA KUSHABIKIA KOMBE LA DUNIA...

“Sisi kama viongozi tunajua nini kinaendelea hao wanaomtaka waendelee tu na sisi taarifa zote tunazo jamani lakini wakumbuke walimshindwa, na tunajua wazi wanafanya hivyo kama kukomoa baada ya kuwatibulia diri la Moses Phiri.”

Sio Morrison wala viongozi wa Yanga uliopatikana kuelezea juu ya madai hayo, licha ya Mghana huyo mapema kabla ya Simba haijatoa taarifa ya kusimamishwa kwake aliandika katika akaunti yake ya mitandao ya kijamii akiwataka wabashiri nini kitakachotokea kwake, huku akiweka picha akiwa na mabegi.

Tangu Morrison aje nchini akijiunga na Yanga amekuwa akitajwa kufanya vituko, ikiwamo enzi akiwa na Yanga aligoma kusafiri na wenzake hadi kukodiwa ndege, pia kutuhumiwa kumtolea kisu mlinzi wa hoteli moja wakati Yanga ikiwa kambini kujiandaa na mechi ya ASFC dhidi ya Kagera, tukio liliripotiwa Julai 2, 2020.