Home news KISA KUTOMUANZISHA CHAMA KWENYE MECHI YA JUZI…MATOLA AJIKUTA MATATIZONI SIMBA…ASHUKIWA KAMA MWEWE..

KISA KUTOMUANZISHA CHAMA KWENYE MECHI YA JUZI…MATOLA AJIKUTA MATATIZONI SIMBA…ASHUKIWA KAMA MWEWE..


SIMBA juzi walipambana na kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza katika mchezo mgumu ulioonekana ungemalizika kwa suluhu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, juzi Jumapili. Hiyo ni siku moja tu tangu vijana wengine wa Mbeya, Mbeya City, wawabane vinara Yanga kwa suluhu pia.

Matokeo hayo yanaifanya Simba, ifikishe pointi 31 katika nafasi ya pili, ikiwa imebakiza pointi tano tu iwafikie Yanga wenye pointi 36 kileleni lakini Simba wakiwa wamecheza mchezo mmoja zaidi.

Kiungo Clatous Chama ‘Mwamba wa Lusaka’ ndiye aliyeleta tofauti kwenye mchezo huo, baada ya kufunga bao pekee dakika ya 80, ambalo lilizua utata mkubwa kufuatia straika Meddie Kagere kuonekana kuotea lakini beki wa Mbeya Kwanza aliugusa mpira kabla haujamfikia Kagere na mwamuzi msaidizi akatafsiri alivunja offside hiyo.

Wachezaji wa Mbeya Kwanza walimzonga mwamuzi msaidizi wakilalamika kuwa hilo siyo bao halali. Msonjo akapewa kadi ya njano kutokana na tukio hilo dk ya 80.

Hii ni mechi ya pili Simba wanapata bao linaloonekana kuwa ni la utata, katika mchezo uliopita ambao pia walishinda 1-0 dhidi ya Prisons, walipata penalti iliyoonekana tata iliyofungwa na Kagere. Kwenye mchezo huo wa juzi, Simba walianza na washambuliaji wawili ambao ni John Bocco na Meddie Kagere huku Clatous Chama akianzia benchi.

Dakika ya 1 tu, Bocco alifanya jaribio ambalo halikuleta matunda na dakika ya 8 na 13, Pape Ousmane Sakho alipiga mashuti yaliyolenga lango huku Rally Bwalya akiwa ni mpishi eneo la kati. Simba katika mchezo wa jana, ilitengeneza nafasi lakini ilikuwa haina ubunifu katika umaliziaji, huku wakipiga mashuti 16 nje ya lango hadi kufikia dakika ya 79.

Kwa Mbeya Kwanza mpishi wao mkuu alikuwa ni Salum Chuku ambaye amekuwa na majukumu ya kupiga kona na mipira ya kurusha. Sadio Kanoute alifanya jaribio kwa kichwa dakika ya 17 lililookolewa na kipa Hamad Kadedi ambaye alikuwa salama ndani ya dakika 15 za mwanzo chini ya beki Rolland Msonjo.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUPOTEZA MATUMAINI YA KOMBE LOLOTE MSIMU HUU...MASTAA SIMBA WAPEWA 'LIKIZO FUPI'...USAJILI WAJA...

Dakika ya 13, Habib Kiyombo nusura aipatie Mbeya Kwanza bao alipofanya jaribio lililookolewa na kipa Aishi Manula. Dakika ya 28, Salum Chuku naye alifanya jaribio lakini likaokolewa na Manula.

Lakini kukosa utulivu kwa nyota wa Simba kuliwafanya washindwe kupata bao ndani ya dakika 40 za mwanzo, pongezi kubwa kwa Hamadi Kadedi kipa wa Mbeya Kwanza pamoja na Rolland Msonjo.

Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisomeka Simba 0-0 Mbeya Kwanza. Mashabiki wa Simba walianza kulalamika mapema walipoona orodha ya wachezaji wa mchezo ‘line up’, baada ya kuona Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama ameanzia benchi.

Mashabiki katika ukurasa wa Instagram wa Simba, wengi walianza kumlalamikia kocha wakisema haikustahili kumuweka Chama benchi. Jana Selemani Matola ndiye aliyekuwa kocha kufuatia Mhispania, Pablo Franco kuendelea kutumikia kifungo chake cha mechi tatu.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Simba ikitengeneza mashambulizi mengi, mapema tu Simba ilimtoa Jonas Mkude na nafasi yake ikachukuliwa na Chama. John Bocco naye alitoka akaingia Chris Mugalu. Dakika ya 54, Kagere atajilaumu mwenyewe kwa kukosa nafasi ya wazi kufunga.