Home news KUELEKEA MECHI NA MTIBWA…YANGA WAPATA PIGO…MOLOKO KUPIGWA KISU..WATANO WANAUGULIA …

KUELEKEA MECHI NA MTIBWA…YANGA WAPATA PIGO…MOLOKO KUPIGWA KISU..WATANO WANAUGULIA …


KIUNGO mshambuliaji kipenzi cha Kocha Mkuu, Nasrredine Nabi, Mkongomani Jesus Moloko, ametakiwa kukaa nje ya uwanja kwa siku 45, baada ya kufanyiwa vipimo huku akitakiwa kufanyiwa oparesheni ndogo ‘kupigwa kisu’.

Kiungo huyo alishindwa kumalizia mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Biashara United uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam hivi karibuni baada ya kupata majeraha.

Moloko ameongeza idadi ya wachezaji wenye majeraha na kufikia watano, wengine ni Chrispin Ngushi, Shomari Kibwana, Yacouba Songne, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Denis Nkane.

Daktari wa Viungo wa Yanga, Mtunisia Youssef Ammar alisema kuwa Moloko atakaa nje kwa muda huo wa siku 45 ambao ni zaidi ya mwezi mmoja na nusu,baada ya kufanyiwa kipimo cha MRI.Ammar alisema kuwa kiungo huyo mara baada ya kipimo hicho, ameonekana kupata maumivu ya misuli katika mguuwake wa kushoto yatakayomuweka nje ya uwanja kwa muda wa siku 45.

Aliongeza kuwa kiungo huyo hivi sasa amepewa mapumziko maalum sambamba na kupatiwa matibabu ya maumivu hayo kabla ya kuanza mazoezi mepesi ya binafsi.

“Moloko atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku 45 sawa na mwezi mmoja na siku 15 baada ya vipimo kubaini alipata maumivu makali ya misuli katika goti lake ambayo hayatamfanya afanyiwe oparesheni kubwa kama ilivyokuwa kwa akina Yacouba (Songne).

“Hivyo tayari haraka ameanza matibabu hayo ya maumivu ili kuhakikisha anarejea baada ya siku ambazo ametakiwa kukaa nje ya uwanja.

“Kuumia kwa Moloko kumeongeza idadi ya wachezaji wenye majeraha na kufikia watano hivi sasa katika kikosi chetu cha Yanga,” alisema Ammar.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI vs AL AHLY KESHO... SIMBA WAFANYA MAAMUZI HAYA MAGUMU...