Home Uncategorized SIMBA YAMPONZA MZUNGU WA AZAM FC

SIMBA YAMPONZA MZUNGU WA AZAM FC

ARSTICA Cioaba,raia wa Romania, Kocha Mkuu wa Azam FC  ametozwa faini ya kiasi cha shilingi laki tano (500,000) kwa kosa la kugoma kuongea na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kukamilika.

Kwenye mchezo kati ya Azam FC na Simba uliohezwa Machi 4, Cioaba aligoma kuongea mara baada ya mchezo kukamilika.

Azam FC walianza kufunga bao dk ya nne halikudumu mpaka mwisho wa dk 90 Simba walipindua meza kibabe na kusepa na pointi tatu kwa ushindi wa mabao 3-2.

Adhabu hiyo ni kwa kuzingatia Kanuni namba 41(12) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha na imetolewa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

SOMA NA HII  KUKAMATWA KWA MZEE KILOMONI KWAWA GUMZO...