Home news KUELEKEA MECHI YA JUMAPILI…MKUDE AMUWAHI MUARABU…MWENDA NAYE ARUDI…

KUELEKEA MECHI YA JUMAPILI…MKUDE AMUWAHI MUARABU…MWENDA NAYE ARUDI…


SIMBA jana ilitua Casablanca tayari kwa safari ya kuifuata RS Berkane mjini Berkane kwa mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku nyota wao, Jonas Mkude na Israel Mwenda wakirejea mapema kuwawahi Wamorocco hao.

Wachezaji hao walishindwa kucheza mchezo uliopita wa Kundi D dhidi ya USGN ya Niger ulioisha kwa sare ya 1-1 baada ya kuugua ghafla, lakini kwa sasa wamepona na wameanza kujifua na wenzao.

Kuumwa kwa Mkude kulifanya akosekane kabisa hata katika benchi, huku Mwenda alikaa tu kwa vile kulikuwa na idadi ndogo ya wachezaji wa akiba na Kocha Pablo Franco alisema ilikuwa ngumu kwenye maandalizi ya mchezo huo ikiwemo kuwakosa wachezaji wake kutokana na kuumwa.

“Ukiangalia katika benchi la akiba kulikuwa na makipa wawili, Ally Salim na Benno Kakolanya, jambo ambalo hata Mwenda alikaa kutimiza idadi ya wachezaji ila hakuwa fiti asilimia zote,” alisema Pablo.

Hata hivyo, Daktari wa Simba, Edwin Kagabo alisema baada ya kuwapatia matibabu wachezaji hao wanaendelea vizuri na baada ya kufika Morocco watafanya mazoezi pamoja na wenzao.

“Mkude na Mwenda wote wapo sawa kiafya tofauti na ilivyokuwa siku moja kabla ya kucheza na USGN, kuhusu kama watatumika kwenye mechi ya RS Berkane hilo ni la kocha lakini wapo fiti sasa,” alisema Edwin.

SOMA NA HII  BAADA YA KUBADILISHANA JEZI NA MESUT OZIL, MBWANA SAMATTA APEWA ONYO UTURUKI..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here