Home news KUHUSU ALIKO PETER BANDA NA HALI YAKE..UONGOZI SIMBA WAANIKA HAYA…WAGUSIA ISHU YA...

KUHUSU ALIKO PETER BANDA NA HALI YAKE..UONGOZI SIMBA WAANIKA HAYA…WAGUSIA ISHU YA MECHI ZA CAF…


SIMBA imeweka wazi kuwa mara baada ya kiungo mshambuliaji wao, Peter Banda kurejea nchini akitokea Cameroon alipokuwa na kibarua cha kuiwakilisha Malawi kwenye mashindano ya Afcon, moja kwa moja atajiunga na programu za maandalizi ya michezo ijayo hususani mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast. 

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba imepangwa kwenye Kundi D pamoja na timu za RS Berkane ya Morocco, USGN ya Niger na ASEC Mimosas.

Mchezo wa kwanza wa Simba katika hatua ya makundi utakuwa Jumapili ya Februari 13 dhidi ya ASEC Mimosas, mwaka huu wakianzia nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti la Championi Ijumaa, Mkuu wa Maudhui wa Simba, Ally Shatry, alisema: “Ni kweli tunamtarajia kiungo mshambuliaji wetu Banda kujiunga na kikosi baada ya kumaliza majukumu yake ya timu ya taifa ambapo mpaka kufikia mazoezi ya jana (juzi), Jumatano jioni alikuwa hajaripoti.

“Tunatarajia atajiunga na kikosi mara baada ya mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons, ambapo atakuwa sehemu ya programu za kujiandaa na michezo yetu miwili inayofuata hususani ule wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas.”

SOMA NA HII  IANZE WIKI YAKO KWA KUSHINDA MTINYO KIULAIINI KUPITIA CASINO YA KENO NDANI YA MERIDIABET..