Home news SAKHO AFUNGUKA KUHUSU BAO ALILOWAFUNGA WAIVORY…ADAI LINAMAANA HII…HAKUWA NA BAHATI….

SAKHO AFUNGUKA KUHUSU BAO ALILOWAFUNGA WAIVORY…ADAI LINAMAANA HII…HAKUWA NA BAHATI….


LILE bao la kideo ambalo alifunga nyota wa Simba, Pape Ousmane Sakho kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast unaambiwa haikuwa bahati mbaya kwa Msenegal huyo.

Wakati Simba ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo huo, Kocha wa Simba Pablo Franco alimuandaa Sakho.

Katika mazoezi hayo karibu wiki nzima, Sakho alionekana kufanya vizuri na mara kadhaa licha ya kufunga mabao mengi makali alifanya majaribio ya kufunga kwa kujibetua ‘tikitaka’ lakini hakuwa na bahati ya kupachika bao, alifanya hivyo siku ya Alhamisi kwenye Uwanja wao wa mazoezi wa Mo Simba Arena. Sakho alisema aina ya ufungaji wake amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara akiwa na timu mbalimbali alizocheza kwao Senegal.

“Bao lina maana kubwa kwa timu kwani tulihitaji kuongoza kipindi cha kwanza na niliitumia vizuri kazi waliyoifanya wachezaji wenzangu hadi kuwa mtu wa mwisho kuweka mpira kambani,” alisema Sakho na kuongeza;

“Simba tunahitaji kufanya vizuri katika mashindano haya na hicho ndio kikubwa tumeingia nacho wachezaji wote ndio maana nilicheza kwa kujituma zaidi.”

SOMA NA HII  MCHEZO WA KIMATAIFA DHIDI YA AL MERRIKH WAMFIKIRISHA GOMES