Home Uncategorized KILE KICHAPO CHA BAO 1-0 WALICHOPOKEA SIMBA KUTOKA KWA YANGA CHAIBUA HAYA

KILE KICHAPO CHA BAO 1-0 WALICHOPOKEA SIMBA KUTOKA KWA YANGA CHAIBUA HAYA


CLATOUS Chama, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa ameumia kwa timu yake kuchapwa bao 1-0 mbele ya Yanga kwenye mchezo wao uliochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa jambo linalomfanya apoteze furaha kama ilivyo kwa mashabiki wa Simba.

Kichapo cha Simba ilichokipata mbele ya Yanga kimewafanya wapinzani wao wafikishe pointi 50 kwenye ligi na mabao 30 huku Simba ikibakiwa na pointi zake 68 na mabao 55.

Chama amesema: “Nimeumia na matokeo mabaya ambayo tumeyapata, sikutarajia kuona haya yanatokea ila mwisho wa siku ni mchezo na tumeyapokea matokeo tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu nyingine,” .

Chama ni kinara wa pasi za mwisho ndani ya Simba akiwa ametoa pasi saba na amefunga mabao mawili.

SOMA NA HII  RATIBA YA LIGI KUU BARA LEO NOVEMBA 28