Home news TRY AGAIN:..HAMTAAMINI…AFUNGUKA HALI YA SIMBA NIGER….AGUSIA ISHU YA KUBWETEKA…

TRY AGAIN:..HAMTAAMINI…AFUNGUKA HALI YA SIMBA NIGER….AGUSIA ISHU YA KUBWETEKA…


SIMBA ipo Niger kuvaana na US Gendarmarie Nationale (USGN), huku mabosi wa klabu hiyo wakitamba kuwa licha ya kukutana na timu wasioifahamu vyema, lakini wanaamini watafanya kweli.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema kuwa anaamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo ujao dhidi ya US Gendarmerie kwa sababu morali ya wachezaji ipo juu na pia kiu yao ya kutaka kuona wanafika mbali katika michuano ya msimu huu.

Simba itashuka uwanjani leo Jumapili katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao hao utakaopigwa Uwanja wa Jenerali Senyi Kountche, huku USGN ikitoka kupasuka Morocco kwa mabao 5-3 na Simba ikiifunga Asec Mimosas ya Ivory Coast kwa mabao 3-1 ikiwa nyumbani – Dar es Salaam.

Try Again alisema anaamini mchezo huo vijana wao watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

Hata hivyo, alisema mchezo utakuwa mgumu kutokana na ugeni wao huko, ila namna morali ya vijana wake ilivyo inampa nguvu za kukiamini kikosi chake.

“Vijana tuwe na imani nao. Wanayajua mashindano ya kimataifa na umuhimu wake. Najua hawatabweteka hata kidogo kwa kuwa nchi inawategemea wao na ndio wawakilishi pekee wa kimataifa hivi sasa,” alisema.

Try Again alisema ameamua kuongozana na wachezaji nchini Niger ili kuongeza nguvu na timu iweze kupata matokeo mazuri.

SOMA NA HII  KISA OFA YA WAARABU....MAYELE AIPA MASHARTI MAGUMU YANGA...ATAKA MSHAHARA MKUBWA ZAIDI...