Home news WAKATI MTIBWA WAKITOA MSIMAMO WAO NI WAPI WATACHEZA NA YANGA..SENZO AIBUKA NA...

WAKATI MTIBWA WAKITOA MSIMAMO WAO NI WAPI WATACHEZA NA YANGA..SENZO AIBUKA NA HILI…

 


YANGA imebakiza dakika 90 dhidi ya Mtibwa kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ambazo wamepania kumaliza kwa kishindo.

Kocha wa Yanga, Nesreddine Nabi ameangalia rekodi zao na Mtibwa akabadilisha ghafla programu za mazoezi ambapo sasa zimefanana na zile za maandalizi ya mechi ya watani kuanzia ndani na nje ya uwanja.

Amewasisitiza mastaa wake kila mmoja akilala akiamka kila muda aufikirie mchezo huo kwani una umuhimu mkubwa kwao.

Hata kwenye kambi yao iliyopo Kigamboni, makocha wamekuwa wakikaa na mchezaji mmojammoja kila mara kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusiana na mchezo huo ambao Simba walilazimishwa suluhu hivi karibuni na kuyumba mechi zilizofuata.

Nabi amepania kukwepa mtego wa suluhu, lakini kuongeza tofauti yao na Simba ambao ni mabingwa watetezi wanaotamba kwamba Yanga imewashikia nafasi yao pale kileleni.

Mechi hiyo itakayopigwa Manungu – Morogoro ina rekodi ambazo zimewashtua Yanga na kulazimika kubadili staili ya mazoezi kuanzia jana watawahi zaidi kufika Morogoro.

Kirekodi Yanga walipokutana na Mtibwa ugenini ndani ya misimu 10 wameshinda mechi mbili pekee huku wenyeji wao wakishinda nne na sare nne.

Rekodi hizo zikawashtua mabosi wa timu hiyo, lakini pia Nabi kisha wakaanza kuchora ramani wakikumbuka kwamba watani wao – Simba waliangusha pointi mbili katika uwanja huo msimu huu.

RAMANI YA NABI

Nabi ambaye uongozi umemhakikishia mkataba mpya wa miaka miwili baadaye mwaka huu, ameanza maandalizi magumu kuanzia juzi akiwarudisha tena wachezaji wake gym wanapojifua kwa saa tatu na nusu. Programu hiyo hufanyika pakiwa na mechi ngumu ya watani.

Jana waliingia katika ratiba ya uwanjani wakianzia asubuhi katika mazoezi makali ya kujaza zaidi ufiti wa mwili kisha jioni wakarudi tena kwa ratiba ya mbinu.

Nabi ameliambia Mwanaspoti kuwa wataingia katika mchezo huo wanaoutazama kama fainali nyingine kutokana na rekodi, lakini ugumu wa wapinzani wao na mapema wanatakiwa kuwa na maandalizi mazuri.

Alisema kwa sasa mbali ya mambo ambayo wameendelea kupambana nayo katika stamina pia wanataka kuhakikisha wanakuwa na ubora mkubwa wa kutumia nafasi ambazo wanatengeneza kazi ambayo itafanyika katika siku tatu kabla ya safari yao ya kuwafuata Mtibwa.

SOMA NA HII  KISA ISHU YA SAIDO NA AMBUNDO KUSIMAMISHWA...MAYELE, SHABANI DJUMA WAJILIPUA YANGA...'WAMFESI' NABI BILA UOGA..

“Tunaiheshimu kila timu. Unajua Yanga kila mechi imekuwa ni kama fainali hatujawahi kuwa na mchezo rahisi. Nimeona hizo rekodi hatuna matokeo mazuri sana ingawa msimu uliopita tulishinda mechi mbili zote,” alisema Nabi akizungumzia mechi hiyo ya Jumatano.

“Ingawa tunakabiliwa na idadi kubwa ya wachezaji majeruhi lakini wapo ambao wanaweza kurejea tutaangalia hizi siku mbili, nimewaambia wachezaji kitu pekee ambacho kitatubeba katika mechi hizi ngumu ni ubora wetu wa kutumia nafasi ambazo tunatengeneza.

“Angalia jinsi tulivyocheza mechi iliyopita niliwapongeza wachezaji wangu kwa jinsi walivyopambana kwa kuwa na kasi kubwa ya kusaka mabao lakini sasa tunatakiwa kuhamia katika kutulia na kuzitumia.”

MSIKIE SENZO

Viongozi nao wamekuwa na hesabu zao na haraka wameshaanza kuufuatilia Uwanja wa Manungu ambao wanakwenda kuutumia kujua mastaa wao watakumbana na changamoto gani wakati wa mchezo.

Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa amesimbs kuwa uongozi wao uko makini kufuatilia maandalizi ya mechi hiyo na kwamba watahakikisha wanakuwa na morali kubwa kwa wachezaji wao kuelekea mechi hiyo.

“Kazi yetu kama uongozi ni kuhakikisha timu inaandaliwa vizuri na hilo linafanyika kule kambini lakini pia tutahakikisha wachezaji wanakuwa katika morali nzuri hili litafanyika, tunajua kwamba mpaka sasa mechi inaonekana itacheza Manungu lakini tuna taraifa kwamba hali ya uwanja ni nzuri labda itokee mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema Senzo.