Home Habari za michezo KUMBE PACOME HAMNA KITU

KUMBE PACOME HAMNA KITU

Habari za Yanga

Wakati Wananchi wakifunga wiki iliyopita kwa kishindo cha pekee baada ya kufanikiwa kuitandika Simba mabao 5-1 katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo.

Kiungo wa Yanga Pacome Zouzoua aligeuka kuwa mada miongoni mwa wapenda soka kutokana na uwezo mkubwa aliouonesha katika mchezo huo huku kila shabiki akisifu uwezo wake.

Sasa habari ni tofauti kwa mchambuzi wa Michezo kutoka TV3, Alex Ngereza ambae anasema kuwa kiwango cha mchezaji huyo ni cha kawaida na sio sahihi kwa mashabiki kumtukuza kupita kiasi.

Akizungumza Ngereza anasema;

“Binafsi sijaona ubora wa kutisha kwa Pacome Zouzoua ni mchezaji wa kawaida tu na amefanya vizuri sana kwenye zile mechi ambazo Yanga wametawala mpira kwa kiasi kikubwa ila mechi ambazo wamepata ugumu yeye pia ameonyesha kiwango cha kawaida sana mfano mechi dhidi ya Namungo na mechi dhidi ya Ihefu siku zote mchezaji bora anafanya vizuri bila kujali ugumu wa mpinzani ila yeye bado anachagua mechi”

SOMA NA HII  KWA MKAPA KUMEDODA...MECHI SIMBA NA YANGA MASHABIKI HAKUNA...ISHU NZIMA IKO HIVI