Home Habari za michezo KAGERA SUGAR WAJA NA MKAKATI MPYA LIGI KUU

KAGERA SUGAR WAJA NA MKAKATI MPYA LIGI KUU

Baada ya ushindi wa mabao 2-1 ilioupata Kagera Sugar dhidi ya Tanzania Prisons, Kocha mkuu wa kikosi hicho, Mecky Maxime amesema wataendelea na mazoezi yao kama kawaida kwa ajili ya kujiweka fiti katika kipindi hiki cha michezo ya kimataifa.

Akizungumza na Mwanaspoti, Maxime alisema ushindi huo ulikuwa ni muhimu kwao baada ya kushindwa kutamba katika michezo miwili mfululizo ila jambo analoendelea kukabiliana nalo ni kutengeneza balansi ya timu kwenye uzuiaji na ushambuliaji.

β€œSio kwa kiwango kikubwa kwa sababu tulishinda ila tunaendelea kuruhusu mabao japo ushindi ndio lengo la kwanza kwetu, tunahitaji mwendelezo wa hilo ili kutengeneza balansi kwenye timu itakayotusaidia katika kila mchezo wetu,” alisema.

Maxime ambaye huo ulikuwa ni ushindi wake wa tatu Ligi Kuu Bara katika michezo tisa aliyocheza, alieleza lengo kubwa la timu hiyo ni kushika nafasi tano za juu na hilo litawezekana endapo tu watakuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo.

β€œKila mmoja wetu ana malengo yake aliyojiwekea na hivyo pia kwetu, msimu huu umeanza na ushindani kwa sababu timu zote zimejipanga vizuri, kadri ambavyo ligi inazidi kusonga ndivyo ugumu nao unaongezeka hivyo ni muhimu kujiandaa mapema.”

Kikosi hicho kitakuwa tena na kibarua kingine kigumu Novemba 22, kwenye Uwanja wake wa Kaitaba itakapoikaribisha KMC.

SOMA NA HII  SALIM ALLY AISHIKA PABAYA SIMBA..... ISHU IKO HIVI