Wakati Yanga wanakubaliana uhamisho wa Kinda Aboubakary Mshery kutoka Mtibwa, walitaka kulipa ada ya uhamisho kwa mikupuo miwili (installments)
Mtibwa walisema wazi kuwa wao wanachotaka ni pesa yote kamili kwakuwa hawana haraka nayo, Mtibwa ikaomba ipewe tarehe maalum ya kulipwa pesa yao yote
Yanga wao walisema pesa yote italipwa DECEMBER 30, Mtibwa walikubaliana na hilo kwakuwa waliwaamini Wananchi na wakakamilisha paperworks zote
Ule muda wa Mtibwa kuingiziwa pesa yao ulipofika haikutumwa hata senti kutoka Yanga, Mtibwa walivumilia kwa wiki mbele kisha kuwapigia kuomba feedback kuhusu malipo
Majibu ya muda wote yalikuwa “tunashughulikia”, “tupo kwenye mchakato” lakini Manungu walisema wapewe tarehe nyingine sahihi ya kuingiziwa pesa yao, Yanga wakatoa tena ahadi
Usiku wa deni haukukawia kukucha, ilipofika tarehe simu hazikuwa zikipokelewa na Viongozi wa Yanga, Mtibwa walituma email, texts WhatApp na simu za kawaida ila hapakuwa na majibu
Katika harakati za kuhitaji mzigo upatikane, CEO alionana na Viongozi wa Yanga, February 23 pale Manungu na mbele ya Mchezaji wakahaidi kulipa siku ya Jumatatu ila ikapita hakuna pesa
Danadana zimekuwa nyingi mpaka hii leo, majibu hayaridhishi kutoka kwa Viongozi wa Yanga na Mtendaji Mkuu wa Mtibwa anakiri wazi kuwa kuna uungwana unakosekana wakati wanapodai haki yao, mara hawaoni emails, mara subirini
Mtibwa wanafikiria Jumatatu wapeleke malalamiko rasmi TFF kuhusu madai yao kutokana na mauzo ya Mchezaji wao
Mtendaji anakiri wazi kuwa licha ya jitihada kubwa za Mtibwa kulea Vijana na kuisaidia nchi lakini kadhia kama hizi zinawaumiza sana Wawekezaji wa Mtibwa na Viongozi, kudai haki imekuwa kama Uadui
Walimruhusu Kijana aende sio kwamba hawakuwa wakimuhitaji ila walikubali ili Kijana atimize ndoto yake, huo ndio uungwana, ni wakati sasa wa Yanga kuwa waungwana.
Credit: Jamiiforum