news

HIVI NDIVYO YANGA WALIVYOTUA DAR KIBABE…HAWATAKI ‘KOKORO NA MTU YANI’… KIBOOSIII KABISA….

admin March 7, 2022 3:00 pm


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Machi 7 kimewasili salama Dar baada ya kuanza safari mapema leo wakitokea Mwanza.

Jana Machi 6,2022 Yanga ilikuwa kwenye msako wa pointi tatu na ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Bao la ushindi lilipachikwa dakika ya kwanza na Fiston Mayele ambaye anafikisha bao la 10 akiwa sawa na Relliats Lusajo anayekipiga ndani ya Namungo FC ya Lindi.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 17 na haijapoteza mchezo hata mmoja.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo ndani ya Yanga na walianza jana kikosi cha kwanza ni pamoja na Paul Godfrey na Sure Boy.

METACHA ATAJWA KIPIGO CHA AZAM…MALALE HAMSINI ASHINDWA KUJIZUIA…AFICHUA SIRI NZIMA… MAYELE AZIDI KUJAZWA NG’OMBE MIKOANI…APEWA MWINGINE MNONO…BUMBULI ATAJA NA MADAFU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply