Habari za michezo

BAADA YA ‘KUFURUSHWA’ NA DODOMA JIJI…MBEYA KWANZA WAMUOKOA MAKATA..KUANZA KAZI LEO..

admin March 21, 2022 7:49 am

 


Baada ya kutemwa na Dodoma Jiji siku chache zilizopita, Kocha Mbwana Makata amejiunga na Mbeya Kwanza kuiongoza katika mechi zilizobaki kuhakikisha anainusuru timu hiyo kushuka daraja.

Mbeya Kwanza ambao ni wageni kwenye Ligi Kuu, hawakuwa na Kocha Mkuu tangu alipotimuliwa Harerimana Haruna Desemba mwaka jana na kukaimishwa Maka Mwalwisi akisaidiana na Nizar Khalfan.

Hadi sasa Mbeya Kwanza wamekusanya pointi 14 na kuwa nafasi ya 15 wakiwazidi alama moja Tanzania Prisons walio mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Meneja wa timu hiyo, David Naftar amethibitisha kutua kwa Kocha huyo mwenye rekodi zake haswa kupandisha timu kadhaa ikiwamo Polisi Tanzania, Alliance FC na Dodoma Jiji akiwa na Msaidizi wake, Renatus Shija.

“Kocha kawasili leo na Msaidizi wake Shija na kuanzia Jumatatu ataanza mazoezi na vijana, tuna matumaini makubwa naye kutuvusha katika mafanikio na kufikia malengo yetu”amesema Naftar.

Naye Makata amekiri kuungana na timu hiyo ya jijini hapa huku akieleza kuwa ataweka wazi mipango yake atakapofika kikosini kujua wapi ataanzia na kuishia.

“Nashukuru nimekaribia, siwezi kuongea chochote hadi nikifika kwenye timu kujua naanzia wapi na kuishia wapi, ishu ya Kocha Msaidizi nalo nitaliongea baadaye” amesema Makata.

Hata hivyo kuwasili kwa Kocha huyo ni kujibu kile kilichoripotiwa na gazeti la Mwananchi hivi karibuni lililoripoti Kocha huyo kuwa miongoni mwa wanaotajwa kujiunga na timu hiyo.

KISA USHINDI DHIDI YA NAMUNGO…KOCHA MSOMALI WA AZAM AWAPIGA YANGA MKWARA WA ‘KUFA NTUU’… KISA KIPIGO CHA JANA…BARBARA ASHINDWA KUJIZUIA SIMBA…ATOA KAULI HII NZITO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply