Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA USGN..UONGOZI SIMBA WATUMA BARUA INGINE CAF…WALIA NA HILI…

KUELEKEA MECHI YA USGN..UONGOZI SIMBA WATUMA BARUA INGINE CAF…WALIA NA HILI…


UONGOZI wa Simba umeweka mikakati mizito kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi na kucheza robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu.

Simba inatarajiwa kushuka dimbani Aprili 3, mwaka huu, wakiwakaribisha Us Gendarmarie katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesisitiza kutumia vema uwanja wa nyumbani kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Alisema wanahitaji ushindi wowote dhidi ya Gendarmarie katika mchezo wao wa mwisho ili kufuzu robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika bila kujali matokeo ya mechi ya RS Berkane dhidi ya Asec Mimosas.

“Tunapeleka maombi Shirikisho la Soka Afrika, CAF, ya kuruhusu idadi kubwa zaidi ya mashabiki, tumepoteza mchezo uliopita lakini hatujapoteza lengo la kutinga robo fainali,” alisema Ally.

Tiketi yetu ya kutinga robo fainali tunayo wenyewe, tunahitaji kushinda tu mchezo wetu bila kuangalia matokeo ya mechi nyingine ndio maana nasisitiza mashabiki kujitokeza kwa wingi Aprili 3 kwa kusapoti timu.”

Alisema mipango yao ilikuwa kuweka rekodi ya kutinga robo fainali ugenini, lakini hawakufanikiwa na sasa wameweka mipango sawa kuhakikisha katika dimba la Mkapa wapinzani wao hawatoki.

Alisema kabla ya kurudi nchini na wachezaji wengine kwenda katika majukumu ya timu za Taifa, viongozi walikutana nao na kukubaliana mechi ya mwisho watapambana hadi jasho la mwisho dhidi ya Gendarmerie ili kutafuta matokeo ya kwenda kucheza robo fainali.

SOMA NA HII  KWA MASHINE HIZI...WABOTSWANA WANATOKEA WAPI ..YANGA YASHTUKIA HUJUMA NZITO..