Home news AHMED ALLY – LIPO WAZI YANGA WANA TIMU BORA..SISI TUNA KIKOSI IMARA…HATUTISHIKI…

AHMED ALLY – LIPO WAZI YANGA WANA TIMU BORA..SISI TUNA KIKOSI IMARA…HATUTISHIKI…


MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amekiri kuwa, watani wao wa jadi, Yanga SC, msimu huu wana kikosi bora tofauti na misimu iliyopita.

Yanga ambayo ipo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 45, safu yake ya ushambuliaji inaongozwa na Fiston Mayele raia wa DR Congo aliyetua kikosini hapo mwanzoni mwa msimu huu.

Katika msimamo huo wa Ligi Kuu Bara, Simba ambao ni mabingwa watetezi, wameachwa kwa alama nane wakiwa nao 37. Timu zote zimecheza mechi 17.

Simba ndani ya misimu minne mfululizo sasa, imefanikiwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara, huku ikichukua Kombe la Shirikisho la Azam Sports mara mbili mfululizo.

Akizungumza jijini Dar, Ally alisema Yanga msimu huu wamechachamaa na kuonesha nia ya wazi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambao waliukosa kwa kwa miaka minne.

Ally alisema licha ya kuchachamaa huko kwa Yanga, lakini wao hawatishiki, kikubwa wanawapa tahadhari na umakini mkubwa katika mbio hizo za ubingwa.

“Lipo wazi kabisa, wapinzani wetu Yanga wana timu bora tofauti na misimu iliyopita na hiyo imetokana na usajili ambao wameufanya.

“Licha ya ubora wao huo, lakini hawatutishi kabisa katika mbio za ubingwa, kikubwa wao wanatupa tahadhari na umakini katika mbio hizi za ubingwa.

“Sisi pia tuna kikosi imara tulichokijenga kwa misimu minne ambacho leo kinaitangaza nchi kimataifa ambacho pia kitatupa ubingwa wa ligi kwa mara tano mfululizo,” alisema Ally.

SOMA NA HII  RAGE : YANGA WAKO VIZURI .....WANASHINDA KWA AJILI YANGU...HAKUNA KAMA MAYELE...