Home Habari za michezo BAADA YA MIEZI MINGI AKIWA WODINI….HATIMAYE YACOUBA HUYU HAPA…APEWA KIBALI …

BAADA YA MIEZI MINGI AKIWA WODINI….HATIMAYE YACOUBA HUYU HAPA…APEWA KIBALI …


Habari njema kwa Wanayanga ni kwamba, mshambuliaji wao, Yacouba Songne muda wowote kuanzia sasa atarejea ndani ya uwanja kuanza kuitumikia timu hiyo mara baada ya kuwa nje kwa kipindi cha takribani miezi mitano akiuguza majeraha ya goti.

Yacouba aliumia katika mchezo dhidi ya Geita Gold Oktoba 2, mwaka jana ambao Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Jesus Moloko ambapo yeye alitoa pasi ya bao hilo.

Akizungumza Daktari wa Yanga, Youssef Amar, alisema Yacouba kwa sasa yupo sawa na kuanzia Aprili 1 ataanza mazoezi.

“Yacouba kwa sasa yupo salama na anaendelea vizuri tofauti na hapo awali ambapo hali ilikuwa mbaya zaidi, kwa sasa tunasubiri mpaka Aprili 1 ndio aanze rasmi mazoezi ya ufiti ambayo ni pamoja na gym.

“Baada ya hapo ataanza mazoezi na wenzake kwa ajili ya kujiandaa kucheza mechi za ushindani ambazo zitakuwa zimesalia msimu huu, tuna imani ataanza kupatikana mapema sana kwa kuwa maendeleo yake ni mazuri,” alisema daktari huyo.

SOMA NA HII  GAMONDI BADO AZAM TU....KWINGINE KOOTE 'KASHALIZWA' KIBABE....