Home news KUELEKEA MECHI NA SIMBA SAFARI HII…NABI KAKUNA KICHWA WEEE…KISHA AKAGUNA NA KUSEMA...

KUELEKEA MECHI NA SIMBA SAFARI HII…NABI KAKUNA KICHWA WEEE…KISHA AKAGUNA NA KUSEMA HAYA…


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema atahakikisha wanashinda mechi zao tatu zijazo kabla ya kuwavaa Simba kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa mwezi ujao, ili kujiweka katika njia ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 42, na mechi zao tatu kabla ya kuivaa Simba ni dhidi ya Geita Gold mkoani Geita, keshokutwa Jumapili, KMC Machi 16, Dar, na Azam FC, Aprili 6, mwaka huu.

Yanga baada ya mechi hizo itaikabili Simba Jumamosi ya Aprili 30, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Nabi alisema kwa sasa wameelekeza nguvu zao katika mchezo wao ujao dhidi ya Geita Gold kabla ya kuanza maandalizi ya michezo inayofuata ambayo itaanza kuwapa taswira ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.

“Sasa tunajipanga na mechi yetu ijayo dhidi ya Geita lakini baadaye tuna mechi mbili ngumu ambazo tunahitaji kupata matokeo kwa aina yoyote kabla ya kucheza na Simba katika mchezo ambao tunaamini utakuwa mgumu zaidi kutokana na kuwaacha kwa pointi nyingi.

“Hatuwezi kufikiria kushindwa kupata matokeo mazuri katika mchezo wetu ambao utatoa mwanga juu ya mechi zetu mbili ambazo tutahitajika kutafuta matokeo bora katika hali yoyote ili tupate uimara katika mchezo mkubwa na wapinzani wetu kuelekea katika harakati za ubingwa ambao ndiyo lengo letu kuu msimu huu,” alisema Nabi.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI