Home Ligi Kuu YANGA WALIVYOPOKELEWA KIFALME MWANZA LEO…GEITA GOLD YAWAHI KUFANYA YAO KIRUMBA MAPEEMAA…

YANGA WALIVYOPOKELEWA KIFALME MWANZA LEO…GEITA GOLD YAWAHI KUFANYA YAO KIRUMBA MAPEEMAA…

 


KIKOSI cha Yanga kimetua leo jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wao wa mzunguko wa pili Ligi Kuu dhidi ya Geita Gold utakaochezwa Jumapili, Machi 6.

Timu hiyo imefika uwanja wa ndege Mwanza saa 5:00 kamili asubuhi na kupokelewa na mamia ya mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi huku wakishangilia na kuamsha shangwe.

Baada ya kupokelewa msafara wa timu hiyo ulielekea katika hoteli ya Antelope iliyopo mtaa wa Mwambani kata ya Ilemela wilayani Ilemela mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kupumzika huku ukisindikizwa na mashabiki wao ambao waliwafikisha hotelini hapo.

Msafara huo ulisimamisha shughuli katika barabara ya uwanja wa ndege kuelekea ilipo hoteli hiyo huku mashabiki wakijaribu kupanda ukuta wa hoteli kuingia ndani kuwaona wachezaji na kuamsha shangwe kwa kucheza wimbo wa ‘Yanga Tamu’ ulioimbwa na msanii Marioo.

Baada ya kupumzika katika hoteli waliyofikia, kikosi hicho kinatarajia kufanya mazoezi baadae jioni kwenye uwanja wa Nyamagana.

Wakati huo huo kikosi cha Geita Gold kilifika Mwanza jana jioni na kufanya mazoezi yao leo asubuhi saa nne katika uwanja wa CCM Kirumba.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUACHWA...NTIBAZONKIZA AIBUKA NA HILI JINGINE KUHUSU YANGA...ATAJA TIMU ATAKAYOCHEZEA MSIMU UJAO...