Home news KUELEKEA MECHI YA KESHO…..AHMED ALLY AFUNGUKA ISHU YA JOHN BOCCO NA HOFU...

KUELEKEA MECHI YA KESHO…..AHMED ALLY AFUNGUKA ISHU YA JOHN BOCCO NA HOFU ILIYOKUWEPO…ATOA OMBI…


NYOTA wa Simba, juzi walianza mazoezi kujiandaa na pambano lao lijalo la michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane, huku mabosi wa klabu hiyo wakiwataja Meddie Kagere, kipa Aishi Manula, Joash Onyango, Hussein Mohammed ‘Tashabalala na Shomary Kapombe pamoja na wazoefu wengine wataibeba kwenye pambano hilo litakalopigwa Jumapili.

Simba inahitaji ushindi kwenye mchezo huo utakaopigwa saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu robo fainali baada ya awali kucharazwa mabao 2-0 ugenini na wapinzani wao hao kutoka Morocco na kuwang’oa kileleni mwa msimamo wa Kundi D.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema jana kuwa uzuri wa kikosi chao kina wachezaji wazoefu wanaofahamu cha kufanya, hivyo hawawezi kumwaambia, Kagere, Kapombe na Manula kitu gani cha kufanya mechi ya nyumbani.

“Wachezaji wote wanafahamu cha kufanya uwanja wa nyumbani na kundi letu, limejijengea tabia hiyo kwa timu zote ndio maana tulivyopata sare ugenini kule Niger dhidi ya USGN ilikuwa kama sherehe ndani yake,” alisema Ally na kuongeza;

“Wachezaji wa Simba morali ipo juu na wanafahamu cha kufanya dhidi ya RS Berkane nyumbani kwani wakishindwa kushinda kwa Mkapa wataenda kushinda kule Benin dhidi ya Asec Mimosa na ni ngumu,”

“Ni mechi yetu lazima tushinde na wachezaji vizuri wanafahamu hilo kwa sababu ndio nafasi pekee ya kushinda.” Katika hatua nyingine Ally alisema kombe hilo kuna timu kubwa zenye ushindani na rekodi kama Pyramids imeshinda mechi zao zote tatu, TP Mazembe na RS Berkane waliowahi kutwaa ubingwa wa michuano hii kwahiyo kuna wakubwa wengine huku.

Ally alisema wachezaji wawili, Clatous Chama atakosa mchezo huo kutokana na kanuni kumzuia pamoja na Hassan Dilunga anayeendelea na matibabu ila wengine wote wapo fiti na tayari kwa mechi.

Alisema hofu ilikuwa kwa John Bocco aliyeshindwa kuendelea na mechi ya Dodoma Jiji ila baada ya kufanyiwa vipimo amegundulika yupo sawa na atakuwa sehemu kwenye sehemu ya maandalizi.

SOMA NA HII  SAMATTA AFUNGUKA 'ALIVYOJIKAZA KISABUNI' NA PESA ZA TP MAZEMBE...ADAI ANGEKUWA CHIZI...

“Kikubwa tunaomba mashabiki wetu 35,000 wajitokeze wote uwanjani kama idadi tuliyopewa na CAF, na muda wote tuishangilie timu yetu ili wachezaji wapate hamasa ya kufanya vizuri.”

Simba ina pointi nne katika kundi hilo ikiwa sawa na Asec Mimosas ya Ivory Coast, huku Berkane ikiwa kileleni na pointi sita na USGN ikiburuza mkia na pointi tatu, huku kila timu ikiwa imeshacheza mechi tatu. Mara baada ya mechi hiyo Simba itasafiri hadi Abidjan, kurudiana na Asec waliyoifumua mabao 3-1 katika mechi yao ya kwanza, mchezo utakaopigwa Machi 20 kabla ya kumalizia kwa kuvaana na USGN, siku ya Aprili 3 na kujua hatma ya kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza nchini kufuzu robo fainali kwa michuano hiyo.