Home Ligi Kuu KUELEKEA MECHI YA LEO…MINZIRO AWAACHIA ‘WAHUNI’ YONDANI NA NYOSSO MSALA WA MAYELE…

KUELEKEA MECHI YA LEO…MINZIRO AWAACHIA ‘WAHUNI’ YONDANI NA NYOSSO MSALA WA MAYELE…


KOCHA mkuu wa Geita Gold, Fred Felix ‘Minziro’ ameendelea kukinoa kikosi chake kuikabili Yanga leo Jumapili hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, huku mabeki Kelvin Yondani na Juma Nyosso wakipewa kazi maalumu ya kumdhibiti kinara wa mabao wa Jangwani, Fiston Mayele.

Mayele anashika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara hadi sasa akiwa na mabao tisa, akitanguliwa na Reliants Lusajo wa Namungo anayeongoza na mabao 10, huku kwenye msimamo Geita ipo nafasi ya saba kwa pointi 20, ilizovuna kwenye mechi 16, ilihali Yanga inayoongoza msimamo kwa pointi 42 kwa mechi 16 pia.

Minziro alisema kwamba, kikosi chake kipo tayari kuikabili Yanga iliyo katika kiwango bora huku akitamba kuwa na wachezaji wazoefu wakiongozwa na Yondani na Nyosso ambao anaamini wataisaidia timu kuondoka na ushindi katika mchezo huo.

“Tutacheza Kirumba, sio uwanja mbaya licha ya kwamba hatujazoea kucheza pale. Ukiangalia kikosi chetu kina wachezaji wengi wazoefu wa ligi hivyo wamewahi kucheza kwenye viwanja vingi tofauti na Kirumba ikiwemo, nadhani uwanja hautakuwa tatizo kubwa kwetu,” alisema Minziro na kuongeza;

“Timu iko vizuri, ukiangalia tangu tumefanya usajiri dirisha dogo tumeimarika karibu kila idara. Licha ya kwamba Yanga ni timu imara lakini na sisi tumeimarika.”

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA