Home news SENZO – YANGA HATURUDI NYUMA…AFUNGUKA VIKWAZO VILIVYOPO…BUMBULI AACHIA TABASAMU…

SENZO – YANGA HATURUDI NYUMA…AFUNGUKA VIKWAZO VILIVYOPO…BUMBULI AACHIA TABASAMU…


KATIKA kuhakikisha wanaendeleza moto wao wa ushindi mfululizo kwenye mzunguko huu wa pili na kufanikisha malengo yao ya kushinda ubingwa, uongozi wa Yanga Jumamosi jioni ulikuwa na kikao kizito cha wadhamini, Kamati ya Utendaji, benchi la ufundi na wachezaji kilichofanyika katika kambi yao ya Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Yanga walimaliza mzunguko wa kwanza wakiwa vinara wa msimamo na pointi zao 39, ambapo juzi Jumapili walivaana na Kagera Sugar kwenye mchezo wao wa kwanza wa mzunguko wa pili uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na kufanikiwa kuendeleza wimbi la ushindi kwa kushinda magoli matatu bila.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha, alisema: “Tumefanya kazi kubwa katika michezo yetu ya mzunguko wa kwanza, tumekuwa na kiwango bora na hili linathibitishwa na rekodi mbalimbali ambazo tumeziandika, kuelekea mzunguko wa pili tunafahamu kuwa tutakutana na wakati mgumu lakini tumedhamiria kutimiza malengo yetu.”

Akizungumzia maandalizi yao ya michezo ya mzunguko wa pili, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Kwanza uongozi unajivunia mafanikio ambayo tumekuwa nayo katika michezo yetu ya mzunguko wa kwanza, ambapo tumemaliza kama vinara wa msimamo tena tukiwa na pengo kubwa kati yetu na wale ambao wanatufuatia.

“Lakini tunajua kuwa mzunguko wa pili utakuwa mgumu maradufu, hivyo kwa kutambua hilo uongozi wa wadhamini wetu, Kamati ya Utendaji, benchi la ufundi na wachezaji kwa umoja Jumamosi jioni tulikutana kuweka mkakati wa pamoja kukusanya pointi tatu katika michezo ya mzunguko huu wa pili ili kushinda ubingwa.

SOMA NA HII  AL AHLY WATUA NCHINI KUIKABILI YANGA, WAPOKELEWA NA HAPPY NATION