Home Simba SC ALICHOSEMA GOMES BAADA YA KAIZER CHIEFS KUTOKA SARE JANA

ALICHOSEMA GOMES BAADA YA KAIZER CHIEFS KUTOKA SARE JANA

 


WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya mabingwa Afrika Simba SC, wapo kamili Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa mzunguko wa kwanza robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs.

Simba watacheza mchezo huo wakiwa na molari ya hali ya juu kutokana na rekodi zao nzuri kwenye mashindano hayo pamoja na Ligi Kuu ya Tanzania na kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Wakati Simba wao mambo yao yakionekana kuwa shwari, upande wa Kaizer Chiefs katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini mambo si mazuri kwao.

Rekodi zinaonyesha Kaizer wamecheza mechi nne za ligi pasipo kuondoka na ushindi wa aina yoyote zaidi ya kuambilia sare na vipigo.

Kaizer Chiefs jana (Jumatano), walicheza mechi ya ligi dhidi ya Swallows wakiwa nyumbani kwao wakatoka sare ya bao 1-1. Kabla ya hapo Kaizer walitoka kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Tshakhuma.

Kabla ya mechi hizo Kaizer wakiwa ugenini walitoka sare ya mabao 2-2 na Bloem Celtic, huku wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa nyumbani kwao bao 0-1, dhidi ya Chippa Utd.

Kocha wa Simba, Didier Gomes anasema Kaizer hawana matokeo mazuri katika ligi ya ndani lakini si timu ya kuibeza na kuona kama mbovu kwani kwenye mashindano ya kimataifa wanabadilika.

“Ukiangalia mechi zao za Ligi ya mabingwa Afrika wanabadilika na kucheza tofauti na mechi zao za ndani pengine ndio maana wapo hapa, tumeliona hilo na tumeandaa plani za kukabiliana nao,” anasema Gomes.

SOMA NA HII  MKUDE YUPOYUPO SANA SIMBA, MKATABA WAKE BADO UNAISHI