Home news SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI ASEC MIMOSAS…WAPIGA TIZI LA KUFA MTU LEO…PABLO ATOA...

SIMBA WAANZA KUIVUTIA KASI ASEC MIMOSAS…WAPIGA TIZI LA KUFA MTU LEO…PABLO ATOA TAHADHARI…


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa Simba chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco wameanza mazoezi ili kuweza kujiweka sawa kwa mechi zijazo za Ligi Kuu Bara pamoja na zile za kimataifa.

 Machi 13,2022 Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Simba 1-0 RS Berkane na kuwafanya Simba kubaki na pointi tatu nyumbani.

Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya ASEC Mimosas unaotarajiwa kuchezwa nchini Ivory Coast walipokutana Uwanja wa Mkapa Simba iliweza kushinda mchezo huo wa awali.

Kwenye kundi D Simba inaongoza ikiwa na pointi 7 baada ya kucheza mechi 4 na wale ambao wanawafuata ASEC wapo nafasi ya pili na pointi 6.

Bao la ushindi kwa Simba lilifungwa na Pape Sakho dakika ya 44 kwa pasi ya Meddie Kagere.

Pablo amesema kuwa baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya RS Berkane hesabu zao ni kwenye mchezo ujao.

“Kila mchezo ambao tunacheza una umuhimu na kwetu sisi ni kuweza kuona kwamba tunashinda, haitakuwa kazi rahisi lakini tupo tayari,”.

SOMA NA HII  MWINYI ZAHERA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA SIMBA