Home news WAKATI WATU WAKIWA NA FURAHA…AHMED ALLY AFICHUA SIRI YA USHINDI JANA..ADAI WASINGETAKATA..

WAKATI WATU WAKIWA NA FURAHA…AHMED ALLY AFICHUA SIRI YA USHINDI JANA..ADAI WASINGETAKATA..


Uongozi wa Klabu ya Simba SC umetoa shukurani kwa Mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam jana Jumapili (Machi 13), kwa ajili ya kushuhudia na kuishangilia timu yao ikicheza mchezo wa Mzunguuko wanne wa ‘Kundi D’, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Meneja wa Habari na Mawasilino Ahmed Ally amesema, bila Mashabiki anaamini timu yao isingetakata kama ilivyoonekana dhidi ya RS Berkane, na kufikia lengo la kuondoka na alama tatu walizozihitaji.

Amesema Mashabiki wametimiza wajibu wao wa kufika Uwanjani, hivyo wachezaji walijua kazi iliyokua imebaki kwao na ndio maana walihakikisha wanaondoka na ushindi uliowaongezea alama kwenye msimamo wa ‘Kundi D’.

“Wamekuja kwa wingi, wametimiza wajibu wao kwa kuishangilia timu yao wakati wote, hii ndio Simba SC tunayoitaka kwa sababu kila mmoja anajua ni wapi mahala pake.”

“Tulihitaji Mashabiki 350000, tunamshukuru mungu wamefika wote bila kukosa, na wao wenyewe wameona kushangili kwao kwa muda wote ndio kuliwachanganya waarabu na kujikuta wanaacha kucheza mpira na kuanzisha vurugu ambazo hazikuleta faida yoyote kwao zaidi ya kuondoka na vilio.” amesema Ahmed

Bao pekee na la ushindi katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Mashabiki 35,0000 lilipachikwa wavuni na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal Pappe Ousman Sakho na kuifanya Simba SC kufikisha alama 07 kwenye msimamo wa kundi D.

Nafasi ya Pili kwenye msimamo wa kundi hilo inashikwa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast yenye alama 06 baada ya kuifumua USGN mabao 2-1, sawa na RS Berkane inayoshika nafasi ya tatu, huku USGN ikishika nafasi ya 04 kwa kumiliki alama 04.

Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa kundi D itaendelea tena mwishoni mwa juma hili (Machi 20), ambapo Simba SC itakua ugenini ikicheza dhidi ya ASEC Mimosas nchini benin, huku USGN ikiikaribisha RS Berkane mjini Niamey-Niger.

SOMA NA HII  KAMA GATOGATO AMEWEZA, KAYOKO NA SASII HAWAWEZI KUSHINDWA