Home Habari za michezo ZIMBWE Jr AKOLEZA CHUMVI KUELEKEA MECHI NA WAIVORY…ATOFAUTIANA NA MABOSI ZAKE SIMBA…

ZIMBWE Jr AKOLEZA CHUMVI KUELEKEA MECHI NA WAIVORY…ATOFAUTIANA NA MABOSI ZAKE SIMBA…


HUKU wakiwa kwenye maandalizi ya mchezo wao wa tano wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas, Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kama wakifanikiwa kufuzu robo fainali ya michuano hiyo, basi watakuwa kwenye nafasi kubwa ya kufika fainali.

Simba inaongoza Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na pointi saba walizokusanya katika michezo minne, wakifuatiwa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast wenye pointi sita sawa na RS Berkane kutoka Morocco, huku US Gendarmerie ya Niger wakibuluza mkia na pointi zao nne.

Jumapili hii Simba inatarajiwa kushuka Stade de l’Amitie nchini Benin, kwa ajili ya mchezo wao wa tano dhidi ya ASEC Mimosas.

Tshabalala alisema: “Tunashukuru kwa nafasi ambayo tupo kwenye msimamo, tumesaliwa na michezo miwili muhimu ambapo tunahitaji kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ili kufuzu hatua ya robo fainali.

“Tunaamini katika ubora ambao kikosi chetu kinaendelea kuuonyesha katika michuano hii, ni wazi kama tutafanikiwa kufuzu robo fainali, basi uzoefu tulioupata msimu uliopita kwenye hatua hiyo utatusaidia kufika fainali.”

Kwa kauli hiyo ni wazi Zimbwe Jr ametofautiana na malengo ya mabosi zake, ambapo mara kadhaa wamekuwa wakinukuliwa kuwa wakisema malengo yao ni kufika nusu fainal ya kombe la shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MAMBO MAZITO...NCHIMBI ATEMANA NA YANGA MAZIMA..UONGOZI WAFUNGUKA HAYA...