Home Habari za michezo KAPOMBE AWA GUMZO AFRIKA KUSINI….MASHABIKI WA KAIZER CHIEFS, MAMELOD WAOMBA JEZI ZA...

KAPOMBE AWA GUMZO AFRIKA KUSINI….MASHABIKI WA KAIZER CHIEFS, MAMELOD WAOMBA JEZI ZA SIMBA…


Licha ya Simba kuwa na mastaa kibao wenye uwezo mkubwa, lakini jina la beki Shomary Kapombe limekuwa gumzo Afrika Kusini wakati timu hiyo ikijiandaa kucheza Orlando Pirates katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Utamu zaidi ni kwamba mashabiki wa Kaizer Chiefs wamewahakikishia Watanzania watakuwa nao bega kwa bega katika mechi hiyo itakayopigwa Jumapili, mjini Soweto na kama Simba itapata sare tu, itatinga nusu fainali. baadhi ya Watanzania wanaoishi Afrika Kusini, akiwamo shabiki wa Simba, Abdallah Mabange waliosema kwa sasa nchini humo Kapombe amekuwa akitajwa zaidi.

Mabange alisema katika mchezo uliopita kuna video ya beki huyo ilisambaa mitandaoni kwao ikionyesha kocha wa Orlando Mandla Ncikazi alivyokuwa akimshangaa kutokana na kazi nzuri aliyoifanya uwanjani.

“Yaani huku Kapombe ndio yuko kwenye vinywa vya mashabiki wa Orlando japo wapo mastaa wengi, Sakho kidogo wanamsema ila huyu beki kazidi kuwa gumzo na sisi tunamsubiri kwa hamu,” alisema.

Mabange alisisitiza kuwa suala la Simba na namna ambavyo watakavyowapokea watakapofika liko mikononi mwao wakishirikiana na mashabiki wa Kaizer Chiefs. “Huku upinzani upo mkubwa sana, yaani ni kama huko tu, hao Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns pamoja na Royal AM mashabiki wao wote wapo pamoja na sisi Simba,” alisema Mabange aliyezungumza kwa niaba ya wenzake.

WAOMBA JEZI

Ili kuhakikisha sapoti inakuwa kweli na yenye uhalisia, mashabiki hao wameutaka uongozi wa Simba, kwenda na jezi za kutosha kwa ajili yao.

Mabange alisema wanatambua jezi ni biashara, hivyo wako tayari kuzinunua ili wawe nazo siku ya mchezo. “Tuna imani kubwa na viongozi watalifanyia kazi kuhakikisha tunapata jezi ambazo zitatutambulisha vyema kama Simba katika mchezo huo,” alisema Mabange na kuongeza kocha wa Orlando, Mandla Ncikazi kulalamika juu ya Simba sio jambo geni na hata katika ligi yao keshazoweleka. “Huyo kocha asiwatishe Simba, hata huku tulishamzoea sana kwa kulalamika, hajawahi kuwa na jema hasa timu yake inapofanya vibaya.”

SOMA NA HII  KISA CAF KUZUIA WACHEZAJI YANGA...GSM AINGILIA KATI...AFANYA MAAMUZI MAGUMU..NABI ATAJWA