Home Uncategorized BANDA: MAMBO MAGUMU HATA HUKU SIO BONGO PEKEE

BANDA: MAMBO MAGUMU HATA HUKU SIO BONGO PEKEE

Abdi Banda azichana Simba na Yanga

ABDI Banda, nyota wa Tanzania anayepiga soka la kulipwa nchini Afrika Kusini amesema kuwa mambo magumu hata huko aliko Afrika Kusini kutokana na Ligi yao kusimamishwa.

Banda anakipiga ndani ya Klabu ya Highlands Parks nafasi yake ni beki ambapo aliibukia Afrika Kusini akitokea Klabu ya Simba.

Kwa sasa anaendelea kufanya mazoezi ndani baada ya Ligi kusimamishwa tangu mwezi Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo linaivurugavuruga dunia.

Banda amesema:”Kukaa bila kucheza kwa muda ni ngumu hata kwetu pia sio Bongo pekee unajua maisha ya mchezaji yanategemea kucheza ila kwa sasa hakuna masuala hayo bado tunachukua tahadhari na kuendelea kufanya mazoezi binafsi.

“Huku kila mmoja amepewa program yake ambayo anatimiza na mwalimu anafuatilia kupitia mitandao ambapo kila mmoja anapaswa atume video yake ili kuendelea kupewa aina nyingine ya mazoezi, ” amesema Banda.
SOMA NA HII  NI MUDA WA KLABU ZOTE BONGO KUUNGANA KWENYE VITA HII, ILE VITA YA AWALI MUDA WAKE UMEISHA