Home Uncategorized HAPA NDIPO WALIPOPISHANA JEMBE NA MAREHEMU RUGE

HAPA NDIPO WALIPOPISHANA JEMBE NA MAREHEMU RUGE


MIONGONI mwa walioleta mapinduzi kwenye muziki wa Bongo Fleva jina la marehemu Ruge Mutahaba halikosekani kutokana na kuwa mpambanaji na muongoza njia huku akiwabadilisha kimuziki watu wengi.

Mfano wa waliopitia kwenye mikono yake ni pamoja na Rachel wa kizunguzungu, Lady Jaydee ambaye awali alikuwa anarap ila Ruge akamwambia abadilike na aimbe, Barnaba Boy, Amin ni orodha ya mfano tu.

Katika orodha hiyo ongeza na jina la Saleh Jembe ambaye kwa sasa ni Mhariri Mtendaji ndani ya Kampuni ya Global Group ila yeye alifanya naye kazi kwa ukaribu na Ruge walipishana kwenye upande wa mtazamo.

Jembe amesema:-Mimi nimefanya kazi na Marehemu Ruge, alikuwa anaupigania sana huu muziki wa rap, lakini tukaja kupishana na yeye baadae, ambapo naye alikuwa anaamini kuwa Hip Hop siyo mziki wa biashara, mimi nikapishana naye hapo kwa sababu kwa upande wangu nilikuwa naamini tofauti,” .

Video kamili ipo ndani ya Globaltv Online.

SOMA NA HII  FAMILIA YAPINGA MAHAKAMANI WOSIA WA MENGI, MAZITO YAIBUKA