Home Uncategorized MCHEZAJI YANGA AAHIDI KUIVUA UBINGWA SIMBA

MCHEZAJI YANGA AAHIDI KUIVUA UBINGWA SIMBA


Baada ya kukamilisha dili la kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, beki Ally Mtoni ‘Sonso’ ameahidi msimu ujao lazima waivue Simba ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Sonso aliyesaini mkataba huo akiwa nchini Misri na kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa kinashiriki michuano ya Afcon, amejiunga na Yanga akitokea Lipuli FC ya Iringa.

Beki huyo mwenye uwezo wa kucheza kushoto na kati, amesema kabla ya kusaini mkataba huo, alizungumza na Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera na kukubaliana kwamba msimu ujao wakifanya kazi pamoja, watachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

“Unajua kwamba kabla ya kusaini mkataba kuitumikia Yanga, nilikutana na Zahera tukazungumza mambo mengi akisema kwamba ananihitaji katika kikosi chake kwa msimu ujao.

“Katika mazungumzo hayo, aliniambia kama nikijiunga na Yanga basi tutakuwa na asilimia kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu ujao, hivyo nimekuja hapa kuhakikisha hilo linatimia,” alisema Sonso.

Hivi sasa ubingwa wa Ligi Kuu Bara unashikiliwa na Simba ambayo imeutwaa mara mbili mfululizo katika msimu wa 2017/18 na 2018/19. Kabla ya hapo, Yanga iliuchukua ubingwa huo kwa misimu mitatu mfululizo 2014/15, 2015/16 na 2016/17.

SOMA NA HII  AZAM FC KUTESTI MITAMBO KUELEKEA MCHEZO WAO DHIDI YA KMC