Home Habari za michezo YANGA vs NAMUNGO…MECHI ‘MFUPA MGUMU’ KWA YANGA….HAWAJAWAHI KUPATA USHINDI DHIDI YA NAMUNGO..

YANGA vs NAMUNGO…MECHI ‘MFUPA MGUMU’ KWA YANGA….HAWAJAWAHI KUPATA USHINDI DHIDI YA NAMUNGO..


Yanga na Namungo kila moja ipo kambini ikijiandaa na pambano la Ligi Kuu Bara baina yao litakalopigwa keshokutwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, huku timu hizo zikitenganishwa na Simba katika msimamo.

Yanga ipo kileleni ikiwa na pointi 51 kutokana na mechi 19, wakati Namungo ipo nafasi ya tatu na alama 29, nyuma ya Simba iliyopo nafasi ya pili na pointi 41.

Utamu ni kwamba katika mechi tano zilizopita Ligi Kuu tangu Namungo ipande daraja 2020 hakuna aliyewahi kutoka na ushindi, kwani michezo hiyo ilimalizika kwa sare ikiwamo pambano la kwanza msimu huu lililopigwa Lindi.

Wakati mechi hiyo ikisaliwa na siku chache kabla ya kupigwa Kwa Mkapa, kuna vita mpya inayaotarajiwa kuibuka katika pambano hilo na hii ni bato ya nyota wa timu hizo ambazo zimekuwa kama zina upinzani flani wa chinichini. Katika mechi ya mkondo wa kwanza, iliyopigwa Novemba 20, mwaka jana Uwanja wa Ilulu, Lindi zilitoka sare ya 1-1, Obrey Chirwa alifunga bao zuri dakika ya 52 na Yanga kuchomoa kwa penalti iliyozua utata, ikizamishwa na Saido Ntibazonkiza dakika ya 81.

Bato linalotarajia kupamba pambano hilo ni ile ya eneo la ushambuliaji dhidi ya mabeki na kiungo lililojaa mafundi watupu na hasa baada ya Khalid Aucho na Yannick Bangala kurudisha pacha yao uwanjani.

Kwa upande wa Yanga kuna Fiston Mayele mwenye mabao 11 na asisti tatu, Saido (mabao 6, asisti 5), Shaban Djuma (mabao 3, asisti 3), huku Namungo ikiwa na Reliants Lusajo mabao 10 na asisti 3, Chirwa (mabao 2, asisti 3) na Shiza Kichuya (mabao 2 na asisti2).

Kutokana na mchango wa mastaa hao, waliouonyesha kwenye timu zao utafanya watengeneze ushindani mkali na wa kusisimua.

Katika mchezo huo, Mayele atatakiwa kutumia mbinu kali zaidi kupenya katikati ya mabeki wa Namungo ambao ni Abdulrazack Mohammed na Frank Magingi wanaonekana kuanza mara kwa mara kikosi cha kwanza.

Huku Saido kama ataanzishwa anayetumia akili, atakutana na kibarua kwa AbdulAziz Makame na Hashim Manyanya wanaotumia nguvu kukaba, jambo litakalofanya bato yao iwe ya msisimko. Kwa upande wa Djuma ajiandae kukabiliana na mbio za Kichuya anayeisumbua Yanga tangu akiwa Simba na mchezo wao wa kwanza aliwakosakosa.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI

Makocha wa timu zote wameeleza kuwa mchezo huo ni mgumu na hautabiriki kirahisi kutokana na matokeo ya mechi zao tano zilizopita, ambapo Nasreddine alisema hiyo mechi kwake ni kama nusu fainali akiisaka mechi ya Kariakoo Derby. “Sio mechi nyepesi, lakini kama tutapata matokeo mazuri itaturahisishia kazi kwa mchezo ujao dhidi ya Simba, nimeshazungumza na vijana wangu tunatakiwa tushinde kama kweli tunataka ubingwa msimu huu,” alisema Nabi.

Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, kocha msaidizi wa Namungo alisema hana presha na mchezo huo, licha ya kujua ugumu ilionao Yanga ambayo msimu huu.

Mechi zilizopita

Mar 15, 2020

Namungo 1-1 Yanga

Juni 24, 2020

Yanga 2-2 Namungo

Nov 22, 2020

Yanga 1-1 Namungo

Mei 15, 2021

Yanga 0-0 Namungo

Nov 20, 2021

Namungo 1-1 Yanga

Apr 23, 2022

Yanga ??? Namungo