Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KARIAKOO DABI…MANARA AWACHIMBA MKWARA WA KIMASAI SIMBA…

KUELEKEA MECHI YA KARIAKOO DABI…MANARA AWACHIMBA MKWARA WA KIMASAI SIMBA…


Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara amesema klabu yake inakusudia kujaza uwanja wa Mkapa kwa angalau robo tatu ya mashabiki watakaojitokeza kuutazamana mchezo huo.

Manara amenadi kuwa kutakuwa na promosheni maalumu ambayo itawahusisha mashabiki wa Yanga ambayo itakuwa ni ya kutoa kiasi cha shilingi 25000 za kitanzania shabiki anapata tiketi ya mzunguko pamoja na jezi ya yanga ya msimu huu unaoendelea au kutoa shilingi 15000 za kitanzania na kuambulia tiketi ya mzunguko pamoja na jezi ya msimu wa 2020/2021.

Msemaji huyo anayesifika kwa maneno mengi amebainisha kuwa kutakuwa na magari maalumu ya matangazo ambayo yatakuwa yanatembea maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kuuza tketi pamoja na bidhaa mbalimbali za klabu hiyo.

Manara pia amevitaja baadhi maeneo maalumu kwa ajili ya uzaji wa tiketi ambayo ni Mbagala, Gongolamboto na Tegeta.

Pambano la Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga na Simba linatarajiwa kufanyika jumamosi hii ya Aprili 30 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Huku kukikwa na kumbukumbu ya sare ya 0-0 wakati miamba hiyo ilipokutana katika hatua ya mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Yanga wataingia katika pambano hilo wakiwa kama wenyeji wa mchezo huku wakiwa wamejikita kileleni wakiwa na jumla ya pointi 54 katika michezo 20 wakifuatiwa na watani wao Simba wenye pointi 41 katika michezo 19.

SOMA NA HII  SIMBA YAANGUKIA KWENYE MTEGO HUU WA FIFA