Home Habari za michezo MANARA AITOA YANGA KWENYE MBIO ZA UBINGWA…AWAPA ‘MAKAVU LIVE’ MASHABIKI WAO…

MANARA AITOA YANGA KWENYE MBIO ZA UBINGWA…AWAPA ‘MAKAVU LIVE’ MASHABIKI WAO…


MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amesema licha ya timu yao kuongoza Ligi mpaka sasa bado hajipi nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa.

Yanga wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 54 kwenye mechi 20 huku Simba wakishika nafasi ya pili wakiwa na 41 kwenye 19.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Manara amesema kihesabu ubingwa upo mikononi mwao lakini kiuhalisia bado wanatakiwa kupambana kukusanya pointi.

Manara amesema jambo kubwa ni kupambana na kuhakikisha wanafikisha pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile.

“Yanga bado haijawa bingwa mashabiki wanatakiwa watambue hilo, tuendelee kupambana kwa pamoja licha ya kutamba msimu ni wetu lakini pointi ndio kitu muhimu,” amesema Manara.

Yanga Aprili 30 watakuwa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya Simba utakaochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni.

SOMA NA HII  KISA MECHI NA AZAM....KISUBI AMUONDOA DIARA YANGA....AMTAKA ASEPE BONGO HARAKA...