Home Habari za michezo PRINCE DUBE ARINGA KISA REKODI YAKE YA KUIFUNGA YANGA BADO INADAI DENI….

PRINCE DUBE ARINGA KISA REKODI YAKE YA KUIFUNGA YANGA BADO INADAI DENI….


MSHAMBULIAJI wa Azam, Prince Dube anajivunia rekodi yake ya kuifunga Yanga ambayo imedumu kwa mwaka mmoja sasa bila ya kuvunjwa.

Rekodi hiyo ni ile ya Aprili 25, 2021, wakati alipoifungia timu yake ya Azam bao 1-0 dhidi ya Yanga ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha Nasreddine Nabi alipoanza kukinoa kikosi hicho na tangu hapo haijawahi kuvunjwa zaidi ya kutoa vipigo na sare.

“Ni jambo nzuri kwangu kuona rekodi ambayo niliiweka mwenyewe haijavunjwa lakini binafsi nilitamani sana kuivunja wakati tulipokutana kwenye michezo yote miwili kwa msimu huu ila bahati mbaya kwangu ilishindikana,” alisema Dube na kuongeza;

“Ni mapema kusema rekodi hiyo haitavunjwa kwa sababu michezo iliyosalia bado ni mingi na lolote linaweza kutokea hivyo tuendelee kusubri na kuona kitakachojiri ingawa kwa sasa akili zangu ni kuisaidia timu yangu kufanya vizuri na wala sio vinginevyo.”

Bao hilo la ushindi kwa Dube lilikuwa la mwisho kwa Yanga kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo imetimia mwaka mmoja sasa bila kuonja ladha ya kichapo, ambapo tangu Aprili 25, 2021, timu hiyo imecheza michezo 27, ikishinda 21 na kutoka sare sita.

SOMA NA HII  AZIZ KI ANOGESHA UJIO WAKE YANGA...AMTUMIA UJUMBE HUU INJINIA HERSI...MASHABIKI WAPAGAWA...