Home Habari za michezo RASMI…YANGA NA AZIZ KI STORI NI KAMA IMESHAISHA…MWENYEWE AFUNGUKA DILI LILIVYO NA...

RASMI…YANGA NA AZIZ KI STORI NI KAMA IMESHAISHA…MWENYEWE AFUNGUKA DILI LILIVYO NA UHAKIKA WAKE..


Mburkinabe Stephane Aziz Ki, anayemalizia mkataba wake na timu ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast, amesema bado yupo katika mazungumzo ya mwisho kabisa na bosi mmoja wa GSM na kila kitu kikimalizika anakuja kuendeleza moto.

Ki, alisema amelazimika kufuatilia ubora wa Yanga na kufurahia kuona timu hiyo ikiwa katika nafasi bora ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao lakini kilichomkosha zaidi ni mzuka wa mashabiki wao maarufu kama Wananchi.

Aliongeza kuwa ameziangalia mechi za msimu huu baadhi za Yanga na kuona ubora mkubwa wa kikosi hicho, akasema anaamini kama mambo yatamalizika vyema, anakuja kujiunga na kikosi chenye ubora mkubwa na wala hana wasiwasi wa nafasi yake.

Aziz Ki aliyeitungua Simba mabao mawili aliongeza kitu zaidi kilichomshtua, ni jinsi mashabiki wa timu hiyo wanavyojaa viwanjani kuipa nguvu timu yao.

“Nilikuwa nimeshtuka sana, wana mashabiki wengi wanaopenda timu yao, niliuliza kila mechi wanacheza nyumbani?Wakaniambia kila sehemu mashabiki wao wapo na wengine wanasafiri kuifuata timu.”

“Ni klabu nzuri na kubwa, kabla nilikuwa siijui lakini waliponifuata nikaijua, nimeifuatilia na kuona naona wanaongoza ligi, nafikiri wanaweza kucheza mashindano ya CAF msimu ujao,” alisema Ki na kuongeza;

“Kitu ninachotaka ni kuendelea kucheza kwa ubora mashindano makubwa kama haya ya Afrika, umri wangu bado unanipa nafasi ya kuwa na ndoto za mbele zaidi, kama watacheza mashindano haya itakuwa ni hatua muhimu kwangu.

“Wanakikosi kizuri (Yanga), napenda wanavyocheza hasa mfumo wao, unakupa urahisi mchezaji kuonyesha uwezo wako, sidhani kama nitakuwa na wasiwasi wa nafasi kama nikija, nitatumia uwezo wangu kucheza.”

Mkali huyo aliyeifungia timu yake mabao matatu katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa kundi moja na Simba, RS Berkane na USGN, aliongeza;

“Hapa nipo kwenye timu kubwa, nafikiri ina rekodi bora kuliko Yanga na nimekuwa napata nafasi, sidhani kama nitashindwa kucheza hapo lakini tusubiri kuona jinsi tutakavyomaliza hili suala pande zote.”

Yanga imeshafanya mazungumzo ya kina na KI, ingawa mwenyewe amekuwa mgumu kutaja kigogo aliyezungumza naye lakini Mwanaspoti linafahamu kwamba Mhandisi Hersi Said, ndiye aliyesafiri mpaka nchini Morocco kumfuata mshambuliaji huyo.

SOMA NA HII  MZIMU WA MOSIMANE WAENDELEA KUISUMBUA AL AHLY...WAINGIA GHARAMA KUBWA KUMPA KAZI "M'BAYA WA CHELSEA"...

Hersi, aliondoka kimafia kimyakimya nchini siku chache kabla ya Yanga kucheza dhidi ya Azam, akimuwahi KI nchini Morocco ambako ASEC ilikuwa ikicheza dhidi ya RS Berkane, katika mchezo wa mwisho wa makundi ya Shirikisho Afrika na usiku wake wakakutana katika moja ya hoteli kubwa mjini Berkane.

Baada ya mazungumzo hayo huku ikielezwa tayari KI ameondoka akiwa amesaini mkataba wa awali Hersi alirudi nchini siku moja kabla ya Yanga kucheza na Azam.

Yanga imepania kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao na kuingia na mziki mnene msimu ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Tayari Tanzania ina uhakika wa kuingiza timu nne kwenye michuano ya CAF mwakani kutokana na ubora wa Simba msimu huu.