Home Habari za michezo SIMBA WALIVYOPOKELEWA KWA ‘VIBE’ LA KICHAGA MOSHI…..MASTAA WOTE FULL MZUKA….

SIMBA WALIVYOPOKELEWA KWA ‘VIBE’ LA KICHAGA MOSHI…..MASTAA WOTE FULL MZUKA….


Kikosi cha mabingwa wa Tanzania bara Simba SC kimefika salama mjini Moshi kikitokea Tanga. Tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji wao Polisi Tanzania mchezo wa Kiporo utakaochezwa Apili 10, 2022. Uwanja wa Ushirika.

Kikosi cha Simba kilicheza mchezo wa Ligi kuu jana April 07, 2022 Jijini Tanga dhidi ya Coastal Union mchezo ambao walishinda kwa ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa katika Dimba la Mkwakwani. Mabao ya ushindi ya Wekundu wa msimbazi kwenye mchezo huo yalifungwa na Bernard Morrison na Meddie kagere.

Mabingwa hao wa Tanzania bara watacheza mchezo wa Ligi Kuu ambao ni wa kiporo dhidi ya Polisi Tanzania ambao ulipaswa kuchezwa Machi 27, 2022. Lakini ulihairishwa kutokana na kuingiliana na kalenda ya kimataifa ya FIFA kabla ya kupangwa kucheza Aprili 10, 2022 Jumapili hii. Na mchezo huu utachezwa Saa 10:00 Jioni Uwanja wa Ushirika Moshi.

SOMA NA HII  SIMBA HESABU ZAO NI MBELE YA YANGA, KWA MKAPA