Home Habari za michezo ZAHERA APATA ULAJI MPYA TIMU YA TAIFA CONGO…ATAMBA KUIPA YANGA MAJEMBE YA...

ZAHERA APATA ULAJI MPYA TIMU YA TAIFA CONGO…ATAMBA KUIPA YANGA MAJEMBE YA UHAKIKA …


KOCHA Mwinyi Zahera amerudishwa tena kuwa kocha wa timu ya Taifa lao la DR Congo akichukua nafasi ya Mkongomani mwingine aliyetemwa katika mabadiliko.

Taarifa iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Congo ni imesema Zahera anarudi katika kikosi hicho kuwa kocha msaidizi akimsaidia Muargentina  Hector Cuper.

Zahera anachukua nafasi ya kocha  Daouda Lupembe ambaye ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata kazi katika timu ya Sanga Balende inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Taarifa hiyo imemtaja kocha huyo anatokea klabu ya Yanga ambapo Zahera alikuwa mkufunzi wa jopo la makocha wa timu za vijana wa timu hiyo ambazo zinafundishwa na wachezaji wa zamani wa timu hiyo.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari, Zahera alithibitisha juu ya uteuzi huo akisema ni hatua nzuri ya kurudi katika majukumu hayo ambapo kwasasa anasubiri kurejea nchini humo kwa kupata muongozo kamili.

Zahera alisema hatua ya uteuzi huo bado itakuwa na faida kubwa kwa klabu yake ya Yanga na kwamba atakuwa anawapa ushauri juu ya wachezaji wazuri wanaoweza kuitumikia timu hiyo.

“Nimepata hizo taarifa ni furaha kubwa kwangu kurudi katika majukumu ya kumsaidia kocha mkuu (Cuper) lakini kikubwa ni kurudisha nguvu ya taifa letu baadea ya kukosa Fainali za Kombe la Dunia,”alisema Zahera.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YAO NA YANGA LEO...MASTAA SIMBA WAVUNJA UKIMYA...WAFUNGUKA HALI ILIVYO KWENYE TIMU...