Home Habari za michezo BAADA YA KUFUNGA GOLI LA KWANZA KWENYE LIGI…MAKAMBO AVUNJA UKIMYA YANGA…KAANIKA YOTE...

BAADA YA KUFUNGA GOLI LA KWANZA KWENYE LIGI…MAKAMBO AVUNJA UKIMYA YANGA…KAANIKA YOTE ANAYOPITIA…


Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo amesema suala la yeye kufunga bao kwenye Ligi Kuu alikuwa amelisubiri kwa muda mrefu, lakini zaidi amefungulia akaunti japokuwa ligi iko ukingoni.

Makambo alifunga bao kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Mbeya Kwanza mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Bao hilo ni la kwanza kwake kwenye Ligi Kuu baada ya kurejea Yanga dirisha kubwa la usajili msimu huu.

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, Makambo alisema kufunga inatokana na nafasi ambayo mchezaji anaipata na sio kwamba hafungi, bali nafasi na suala la muda.

“Mimi nimefunga kwenye FA (Kombe la Azam) na huku kwenye ligi, imani yangu ni kwamba nitaendelea kufunga mechi zijazo,” alisema.

“Nitaendelea kupambana kwenye mechi zijazo na nitafunga tu. Hapa nina furaha kama mchezaji kufunga.”

Makambo msimu wa 2018/2019 alifunga mabao 17 kwenye ligi na kuondoka kwenda nchini Guinea katika klabu ya Horoya, lakini msimu huu amerejea kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na timu hiyo.

Baada ya kurejea Yanga, mchezaji huyo aliingia pamoja na Fiston Mayele ambaye kocha Nassredine Nabi ameonyesha kumuamini zaidi na hajamuangusha baada ya kufunga mabao 13 katika Ligi Kuu.

SOMA NA HII  ODDS ZA USHINDI KWA 'GAME' ZA LEO HIZI HAPA....HAKIKISHA MKEKA WAKO UNASOMA HIVI..