Football ni mchezo unaochezwa kwa kwa ushirikiano wa wachezaji 11, kila mchezaji anapaswa kutoa mchango wake ili kufikia malengo ya timu ambayo ni kupata ushindi.
Ukimuangalia Sakho kiungo Mshambuliaji wa Simba kuna muda anaamini sana kwenye uwezo binafsi (individual skills) kuliko kucheza kitimu zaidi.
Matokeo yake ni kwamba kuna nafasi ambazo anazipata baada ya kuifungu ngome ya timu pinzani lakini anashindwa kutengeneza jukwaa ya ajili ya wachezaji wengine wa simba kufunga.
Ni mchezaji mwenye footwork nzuri lakini Changamoto yake ni hiyo ya kuwa mbinafsi sana linapokuja suala la kucheza kitimu.Siku zote malengo ya timu ndio jambo la kwanza kuliko malengo binafsi.
Ukiangalia juzi kwenye mchezo wa Geita Gold dhidi ya Simba kuna muda Sakho alikuwa anafanya mchezo wa soka kuonekana ni mchezo mgumu.
”Playing football is very simple,but playing Simple football is the hardest thing there is” Johan Cruyff.