Home Habari za michezo AHMED ALLY : KAGERA SUGAR LAZIMA WAPITIE MACHUNGU TULIYOKUTANA NAYO KWAO KAITABA…

AHMED ALLY : KAGERA SUGAR LAZIMA WAPITIE MACHUNGU TULIYOKUTANA NAYO KWAO KAITABA…


Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ameonesha kukumbuka machungu ya kupoteza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar, katika Uwanja wa Kaitaba mwezi Januari 2022.

Simba SC ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0, likifungwa na Mshambuliaji kutoka Uganda Hamis Kiiza Diego na kuifanya klabu hiyo kuwa katika wakati mgumu wa kutetea ubingwa wa Ligi Kuu.

Ahmed ameonyesha kumbukumbu hiyo kwa kuandika ujumbe katika kurasa zake za mitandao ya kijamii (Instagram na Facebook), akithibitish bado hawajasahau machungu waliyosababishiwa na Kagera Sugar.

Ahmed Ameandika: Maangamizi kwa Ruvu Shooting yamemalizika (Al hamdulillah)

Sasa tunaanza maandaliizi ya kumnyoa Kagera Sugar Ni Jumatano Insha Allah saa 1:00 Jioni,

Bado hatujasahau machungu waliyotusababishia nyumbani kwao Bukoba

Ni Wakati wa wao pia kupitia machungu tuliyopitia sisi

Malengo yetu ni kumaliza ligi kwa kushinda mechi zote zilizosalia Insha Allah 🙏🙏

Ushindi ni furaha kwa mashabiki wetu hivyo ni muhimu kushinda kwa ajili yao

SOMA NA HII  AHMED ALLY WA AZAM TV AKABIDHIWA 'FUPA' LA MANARA SIMBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here