Home Habari za michezo BAADA YA KUSAINI MIAKA MIWILI…BEKI MPYA YANGA ALIYEKIPIGA NA THIERY HENRY..AMNYOOSHEA KIDOLE...

BAADA YA KUSAINI MIAKA MIWILI…BEKI MPYA YANGA ALIYEKIPIGA NA THIERY HENRY..AMNYOOSHEA KIDOLE AUCHO…


BEKI wa kushoto wa timu ya taifa ya Uganda, Mustafa Kiiza, ambaye amemalizana na Yanga, amewataja wachezaji Hamisi Kiiza na Khalid Aucho kuwa sababu ya yeye kushawishika kujiunga na klabu hiyo.

Kiiza ambaye alikuwa akikipiga katika Klabu ya Montreal ya nchini Marekani, kwa sasa ni mali ya Yanga mara baada ya wakala wake kuthibitisha kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo.

Kiiza alisema kuwa uwepo wa Khalid Aucho ndani ya Yanga na Hamisi Kiiza ndani ya ligi ya Tanzania ni ushawishi mkubwa yeye kujiunga Yanga.

“Kwa kiasi kikubwa uwepo wa Khalid Aucho na Hamisi Kiiza huko Tanzania umechangia mimi kushawishika kujiunga na Yanga, Hamisi ni kama ndugu yangu na kwa kiasi kikubwa tumekuwa tukiwasiliana juu ya mambo mbalimbali.

“Aucho pia ni rafiki yangu na tumekuwa tukiwasiliana kwa karibu na kama ambavyo unafahamu, Aucho ni mchezaji wa Yanga ambaye amekuwa akinieleza mambo mengi kuhusu timu hiyo, hivyo unachotakiwa kufahamu kwa sasa kila kitu ni kama kimekamilika hivyo tusubiri tuone nini kitatokea huko mwishoni,” alisema beki huyo.

SOMA NA HII  BETI BURE NA MCHONGO MPYA WA MERIDIANBET ....ISHU NZIMA IKO NAMNA HII...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here